Je, Umetanguliza Nini Akhera Ewe Muislamu?
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ))
((Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Anazo khabari ya mnayoyatenda)) [Al-Hashr: 18]
Qiyaamah katika Qur'aan kimetajwa kwa majina mengi. Baadhi ya wataalamu wameona kwamba ni takriban majina thalathini na moja. Miongoni mwa hayo majina ni; Ghad (kesho), As-Saa'ah (Saa), At-Taghaabun (siku ya hasara), Yawmul-Ba'ath (Siku ya kufufuliwa), Yawmul-Aakhirah (Siku ya Akhera), Yawmud-Diyn (siku ya Dini), Yawmul-Faswl (siku ya hukumu), Al-Waaqi'ah (tukio), Yawmul-Wa'iyd (siku ya makamio) na kadhalika.
قال الإمام أحمد: عن المنذر ابن جرير، عن أبيه قال: كنا عند رسول الله صلى الله عليه وسلم في صدر النهار، قال: فجاءه قوم حُفَاة عُراة مُجْتَابي النمار-أو: العَبَاء-مُتَقَلِّدي السيوف عامتهم من مُضَر، بل كلهم من مضر، فتغير وجه رسول الله صلى الله عليه وسلم لما رأى بهم من الفاقة، قال: فدخل ثم خرج، فأمر بلالا فأذن وأقام الصلاة، فصلى ثم خطب، فقال:
(( يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُواْ رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ)) إلى آخر الآي ((إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا)) ( النساء: 1 ) وقرأ الآية التي في الحشر: (( وَلْتَنْظُرْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ لِغَدٍ) تَصَدَّق رجل من ديناره، من درهمه، من ثوبه، من صاع بُرِّه، من صاع تمره -حتى قال-: ولو بشق تمرة". قال: فجاء رجل من الأنصار بصُرة كادت كفه تَعجز عنها، بل قد عجزت، ثم تتابع الناس حتى رأيت كومين من طعام وثياب، حتى رأيت رسول الله صلى الله عليه وسلم يتهلل وجهه كأنه مُذْهبة، فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَن سَنَّ في الإسلام سنة حسنة، فله أجرها وأجر من عمل بها بعده، من غير أن يَنقُص من أجورهم شيء، ومن سَنَّ في الإسلام سنة سيئة، كان عليه وِزْرُها ووزر من عمل بها، من غير أن ينقص من أوزارهم شيء)) أخرجه مسلم من حديث شعبه، بإسناد مثله
Imaam Ahmad amenukuu kwamba Al-Mundhir bin Jariyr amesimulia kwamba baba yake amesema: "Tulipokuwa na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika nyakati za asubuhi mapema, baadhi ya watu walikuja ambao walikuwa hawakuvaa viatu, uchi, walivaa nguo zilizochanika chanika au majoho. huku wamebeba panga zao shingoni mwao. Wengi wao, bali wote walikuwa ni kutoka kabila la Mudhwar. Uso wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ulibadilika rangi alipoona hali ya umasikini wao. Akaingia nyumbani kwake kisha akatoka na kumuamrisha Bilaal aadhini. Alipokwisha adhini na kukimisha Swalah, Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliswalisha kisha akawahutubia watu na kusoma:
((يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُواْ رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ))
((Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi Aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja)) [An-Nisaa:1]
Akasoma mpaka mwisho wa ayah ((Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni)) kisha akasoma ayah hii katika Suratul-Hashr:
(( وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ))
(( na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho))
Akaja mtu mmoja akatoa dinaar yake, dirham yake, kutoka nguo zake, kutoka Sa' (kibaba) yake ya ngano na Sa' ya tende mpaka akasema, "hata ikiwa ni nusu tende". Kisha mtu mwingine miongoni mwa Answaar akaja na mfuko wa pesa mikononi mwake ambao ulikuwa mzito hadi alishindwa kuubeba. Kisha watu wengine wakafuatilia moja kwa moja (kutoa walivyoweza kutoa) hadi nikaona milima miwili ya vyakula na nguo. Nikaona uso wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم uking'ara
Hivyo jiulize Muislamu, je, wewe umetanguliza nini Akhera? Umetanguliza Swalah zako sawa sawa? Umetanguliza Swalah za Sunnah? Umetanguliza Zakaah? Umetanguliza Sadaka? Umetanguliza Swawm? Umetanguliza Hajj? Umetanguliza 'Umrah? Umetanguliza kusoma Qur'aan kwa wingi? Umetanguliza wema wa aina yoyote?
Kumbuka kwamba chochote utakachotanguliza chema basi bila shaka utakwenda kukikuta kinakusubiri malipo yake siku ya Qiyaamah kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى :
((وَأَقِيمُواْ الصَّلاَةَ وَآتُواْ الزَّكَاةَ وَمَا تُقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللّهِ إِنَّ اللّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ))
((Na shikeni Swalah na toeni Zakah; na kheri mtakazo jitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Anayaona mnayoyafanya)) [Al-Baqarah: 110]
************
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


