Kuku Wa Sosi Ya Nyanya Na Dania

Vipimo
Mafuta 4 vijiko vya supu
Kuku 3 LB
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Dania ya unga 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha chai
Bizari ya manjano 1 kijiko cha chai
Uzile 1 kijiko cha chai
Garam masala ½ kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyokatwakatwa 1 au 2
Ndimu 1 kijiko cha supu
Nyanya ya kopo 1 kijiko cha supu
Kotmiri 2 Vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Mkate kuku vipande vikubwa vikubwa, msafishe kwa siki atoke harufu
2. Mrowanishe na vitu vyote isipokuwa ndimu na nyanya ya kopo kwa muda wa nusu saa au zaidi.
3. Mtie katika sufuria na mweke jikoni mpaka awive karibia na kukauka mtie nyanya ya kopo na ndimu mwache kidogo kisha muipue.
4. Mpange kwenye sahani kisha mpambie na vitunguu au chochote.
Kidokezo : Nzuri kula na wali
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


