Nyama Ya Ng'ombe Ya Kkukaanga Na pilipili Manga

Nyama Ya Ng'ombe Ya Kkukaanga Na pilipili Manga

Vipimo 

Nyama ng'ombe -  ½ lb 

Kitunguu - 1 

Kidonge cha supu - 1 

Chumvi - Kiasi 

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai  

Bizari ya pilau (cumin)  - ½ kijiko cha chai  

Mafuta -  2 vijiko vya supu  

Kitunguu saumu/thomu - 1 kijiko cha chai  

Tangawizi  - ½ kijiko chachai   

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

1.   Katika sufuria, kaanga vitunguu mpaka viwe rangi ya hudhurungi  

2.   Tia kitunguu thomu, tangawizi, bizari ya pilau, pilipili manga, kidonge cha supu, na nyama.

3.   Kaanga kidogo kisha tia maji kiasi tu cha kuivisha nyama.   

4.  Funika moto mdogo mdogo mpaka iwe kavu, ikiwa haikuiva utaongeza maji kidogo mpaka ikaangike na tayari kwa kuliwa. 

 

 

 

                 

Share