Qur-aan Ina Roho Na Imeumbwa?

 

Qur-aan Ina Roho?  Imeumbwa?

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalaam alaykum ama baada ya salaam anpenda kumshukuru Allah (SW) na kutakia rehma Mtume wetu Muhammad (SAW) na napenda kuwashuru waislam wote wanashiriki kujibu maswali yetu haya kwani hakutuna la kuwalipa bali Allah ndie atayewalipa inshaallah. Swali langu lipo hapa kuna baadhi wa watu wanasema Qur'an in roho. Je ni kweli ina roho au haina?

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Nabiy, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wasallam) baada ya kumtaja Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kiuvivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.

 

 

Kwa vile Qur-aan si kiumbe. Lakini kama unakusudia maana ya neno la 'ruwhan' ambalo kwa matamshi yetu ya Kiswahili husomeka kuwa ni 'roho' katika Aayah ifuatayo:

 

 وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾

Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh (Qur-aan) kutoka amri Yetu. Hukuwa unajua nini Kitabu wala iymaan, lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.  [Ash-Shuwraa: 52]

 

‘Ulamaa Wafasiri wa Qur-aan, wamekhitilafiana kuhusu maana ya kauli hiyo. Kuna waliosema ni 'Unabiy, kama Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa). Wengine wamesema ni ima Qur-aan au Jibriyl au Wahyi. Wengine wamesea kuwa ni 'uhai' kwa sababu ni uhai unaofisha ujahili.  [Al-Qurtwuby]  

 

Hivyo fahamu kuwa Qur-aan si kiumbe ili kiwe na moyo. Kusema hivyo ni kinyumea na ‘Aqiydah wa Ahlus-Sunnah wal Jamaa’ah na ni kukufuru kama walivyosema ‘Ulamaa.

 

Kwa faida ziyada bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Shaykh Fawzaan: Makundi Mengineyo Yanayodai Kwamba Qur-aan Imeumbwa

Imaam Atw-Twabariy: Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah Hayakuumbwa

Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Qur-aan – 01

 

Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa'ah Kuhusiana Na Qur-aan – 02

 

Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Qur-aan – 03

 

Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Qur-aan – 04

 

Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Qur-aan – 05

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share