Kuku Wa Kuoka Na Viazi Kwa Sosi Ya Hardali

Kuku Wa Kuoka Na Viazi Kwa Sosi Ya Hardali

Vipimo 

Kuku - 1

Viazi - 3

Tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Sosi ya hardali (Mustard) - 1 kijiko cha supu

Mtindi (Yoghurt)  - ¼ kikombe

Kitunguu - 1 kata slaisi kubwakubwa

Pilipili boga (capsicum) - ½  rangi mbali mbali

Chumvi - kiasi

Pilipilipili nyekundu ya unga -  ½ kijiko cha chai

Bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha chai  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Kata kuku osha achuje maji. Weka katika bakuli kubwa.
  2. Changanya katika kibakuli, tangawizi, thomu, sosi, mtindi, pilipili unga, chumvi, bizari.
  3. Mwagia katika kuku. Roweka kwa muda kiasi saa au zaidi.
  4. Menya viazi katakata slaisi za duara.
  5. Katakata pilipili boga (capsicum) za rangi mbali mbali; kijani, manjano na upendavyo.
  6. Changanya viazi katika kuku. Weka kuku katika treya au bakuli la kupikia katika oven.  Oka (bake) kwa muda wa dakika 45 kwa moto wa kiasi.
  7. Epua changanya na pilipili boga na vitunguu. Rudisha katika oven muda mdogo tu viive vitu vyote huu ukichanganya ili vikolee sosi.
  8. Epua, weka katika chombo cha kupakulia ikiwa tayari.   

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share