Nimeambiwa Nina Jini La Kiislamu Kwa Sababu Ya Kupenda Sana Dini

SWALI:

 

Asalam alhkum

nilikuwa nauliza mie nakuwa na hamsha sala ya al-farj na pia nakuwa naota ndoto za dini na nakuwa namsukumo sana kwenye dini,nikienda kuuliza kwa watu wenye elim wanasema tatizo langu nina jin wa kislamu ,nimessomewa dua nyingi lakini naona bado yuko je hawa majini wa kislamu wanarusiwa kuwa na binadamu?


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Bila shaka majini wanawaathiri wanadaamu, pia huenda wakati mwengine jinni akamuingia katika kiwiliwili cha  mwanaadamu kwa kumpenda –ishq- au kwa lengo la kumuudhi, au kwa sababu na lengo lolote jengine, na jini huweza kuzungumza kutokea ndani ya nafsi ya mwanaadam na kuzungumza na anaelewa namna ya kumsomea na kusemesha, na jambo lililo muhimu na lenye kutakikana ni mtu kujikinga na na majini kwa kusoma Ruqyah kutoka katika Qur-aan na Sunnah yenye kupelekea kujilinda nao kama kusoma Aayaatul Kursiy, kwani Aayah hii ikisomwa katika usiku mtu hubakia chini ya hifadhi ya Allaah na hakuna njia ya Shaytwaan kukaribia mpaka kupambazuke, na Allaah ni Mwenye kuhifadhi. Vilevile kuna Aayah zingine mbalimbali na Adhkaar zilizothibiti kama utakavyoona katika viungo vifuatavyo hapa chini:

 

Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

 

Hirizi Inafaa Kuvaliwa Kutibu Maradhi Ya Nafsi Na Jini?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share