Anapotajwa Allaah Atukuzwe Vipi?

Anapotajwa Allaah Atukuzwe Vipi?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

Assalam aleikum wa Rahmatullahi wa barakatuh. Niliuliza Swali hili kwa watu wingi lakini wote hawajuwi. Swali lang ni mtu akisikia Mtume Muhammad (S.A.W) akitajwa watu wasema “Allahumma Swalli wa Sallim alayhi.”  Je, nini la kusema anapotajwa Allaah (S.W.T)?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza tunapenda kukunasihi kutokufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo yenye faid:

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah: Haijuzu Kufupisha Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Maandishi

Al-Lajnah Ad-Daaimah: Haijuzu Kufupisha Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Maandishi

Hukmu Ya Kufupisha Thanaa (Kumtukuza Allaah) Na Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Na Maamkizi Ya Kiislam

 

Kuhusu Swali lako ni kwamba Anapotajwa Allaah inapaswa Atajwe kwa kutukuzwa kwa njia mbali mbali, miongoni mwazo ni zifuatazo: 

 

  • Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)
  • Allaah ('Azza wa Jalla)
  • Allaah (Jalla Jalaaluhu)
  • Allaah (Tabaaraka Wa Ta’aalaa)

Au pia kwa  kumtukuza Allaah kwa njia nyingine yoyote kama ilivyopokewa kwa Athari  zilizo sahihi.

 

Na anapotajwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inapaswa kumswalia kwani kutokumswalia ni aina ya ubakhili kama alivyosema katika Hadiyth:

 

وعن علِيٍّ رضي اللَّه عنْهُ قال: قال رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: ((الْبخِيلُ من ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَم يُصَلِّ علَيَّ)) رواهُ الترمذي وقالَ : حديثٌ حسنٌ صحيحٌ .

Imetoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Bakhili ni yule ambaye nimetajwa kwake na hakuniswalia)) [At-Tirmidhiy na kasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

   

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share