Kusoma Tawassul Kwa Kutaja Majina Ya Allaah 99 Inafaa?

 

SWALI:

 

Asalam Aleikum, shukran sana kwa hii nakala ya Al-hidaya, Inshallah Mungu Atawapa jaza yenu. Swali langu ni hii, hii kusoma tawasulli ambayo watu wanataja majina 99 ya Mwenyezi Mungu Subhanna WaaTalla ni vizuri?

 


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kusoma Tawassul kwa kutaja majina 99 ya Allaah. Tufahamu kuwa hakuna mas-ala ya Muislamu kusoma Tawassul, linahitajika ni wewe kumuomba Allaah Aliyetukuka kwa kuyatumia majina hayo kwa mahitaji yako unayotaka. Kwa minajili hiyo, Allaah aliyetukuka Anasema: “Sema: Mwombeni Allaah, au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye Ana majina mazuri mazuri” al-Israa’ [17]: 110). Na Anasema tena Aliyetukuka: “Na Allaah Ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanaoharibu utakatifu wa majina Yake. Hao watakuja lipwa waliyokuwa wakiyatenda” (al-A‘raaf [7]: 180).

 

Kwa njia hiyo, Muislamu anatakiwa anapomuomba Allaah Aliyetukuka aanze kwa kumsifu na kisha kutaja Majina Yake mazuri kama Ee Allaah, Ee Rahman, Rahiym na majina mengine kabla ya kutaja haja yake.

 

Kwa hiyo, ni juu yetu kama Waislamu kumuomba Allaah Aliyetukuka kwa kuyataja majina yake Mazuri kabla ya kumtaka tunayotaka. Wala si sawa kuyaimba Majina Yake kwa njia ya pamoja au kwa mtu mmoja mmoja kwani hilo sio lengo la Majina hayo.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Kusoma Majina Ya Allaah Kwa Idadi Maalum

 

Je, Majina 99 Ya Allaah Kazi Yake Ndio Hii?

 

Du'aa Gani Asome Mkewe Apate Kizazi? Je, Kusoma Majina Allaah Mara Kadhaa na kupuliza Katika Maji Inafaa?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share