Kababu Na Vitunguu, Nyanya Za Kuchoma (Grilled)

Kababu Na Vitunguu, Nyanya  Za Kuchoma (Grilled)

Vipimo  

Nyama ya kusaga - 2 Lb 

Kitunguu maji kilichosagwa - 1 

Tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu 

Kitunguu saumu/thomu iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu 

Kotmiri iliyokatwa katwa - 1 kikombe 

Maji ya ndimu - 1 Kijiko cha supu 

Mtindi - 2 Vijiko vya supu 

Garam masala - 1 Kijiko cha supu 

Pilipili mbichi iliyosagwa - 2 

Chumvi - Kiasi 

Unga wa dengu - ¼ Kikombe 

Mafuta ya kupakiza wakati wa kuchoma - Kiasi                                    

Nyanya nzima - 3 

Vitunguu vizima - 3   

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Saga nyama mara mbili iwe laini, kisha changanya vitu vyote isipokuwa kotmiri bakisha kidogo na unga wa dengu tia kijiko kimoja kimoja na huku unakanda na kukisia unga.
  2. Funika bakuli na weka ndani ya firiji kwa muda wa saa moja.
  3. Toa mchanganyiko firijini na ugawanye vifungu sawa .
  4. Kisha paka mafuta kwenye mikono na uvingirishe mchanganyiko kutengeneza umbo la kababu kama kwenye picha.
  5. Halafu kata nyanya na vitunguu vipande viwili.
  6. Na uchome (grill) pamoja na kababu kwenye jiko la mkaa huku ukigeuza mpaka zigeuke rangi na kuiva.  
  7. Zikishakuwa tayari ziweke kwenye sahani pamoja na nyanya na vitunguu vilivyochomwa na tupia kotmiri uliobakisha na itakuwa tayari kuliwa.

 

 

Share