Kachori Za Viazi Vya Madonge

Kachori Za Viazi Vya Madonge

Vipimo

Viazi - 12

Chumvi - kiasi

Pilipili ya unga - 2 Vijiko vya supu

Ndimu - kiasi

Unga wa dengu - 1 Kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha viazi na maganda yake.
  2. Vikisha wiva menya maganda na kata kila kiazi vipande viwili.
  3. Katika kibakuli koroga ndimu, chumvi na pilipili ya unga kisha pakaza katikati ya kiazi halafu gandanisha na kipande cha pili kiwe kama kiazi kizima.
  4. Fanya hivyo kwa viazi vyote vilivyobaki.
  5. Kwenye bakuli jengine koroga unga wa dengu , maji na chumvi kiasi uwe kama uji mwepesi.
  6. Kisha chovea kila kiazi kwenye unga huo halafu kaanga kwenye mafuta ukigeuza kama sambusa hadi kuiva.
  7. vikisha wiva panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

 

Share