Katelesi Za Mviringo Za Nyama (Potato Chops)

VIPIMO
Viazi 3 LB
Nyama 1 LB
Unga wa mkate (Breadcrumbs) 1 kikombe cha chai
Mayai 2-3
Mafuta ya kukaangia Kiasi
VIPIMO VYA NYAMA
Tangawazi mbichi na thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Chumvi Kiasi
Jeera (Bizari ya pilau ya unga) 1 kijiko cha chai
Dania (Gilgilani ya unga) 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga ¼ kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Ndimu au limau 2 vijiko vya supu
Kotmiri iliyokatwakatwa (chopped) ½ kikombe cha chai
Kitunguu kilichokatwa katwa (chopped) 1 Kikubwa
NAMNA YA KUTAYARISHA
1.Chemsha Viazi, vikiwiva menya maganda na viponde.
2.Weka nyama katika sufuria ndogo, ichanganye na vitu vyake vyote isipokuwa kotmiri na vitunguu.
3.Ipike nyama mpaka ikauke.
4.Tia Kotmiri na vitunguu viliyokatwakatwa, changanya weka kando.
5.Chukua viazi viliyopondwa fanya donge la kiasi katika mkono wako kisha fanya shimo.
6.Teka nyama kwa kijiko cha chai na tia katika shimo la viazi na rudia kulifanya donge kwa kuifunika nyama na viazi. Weka kando.
7.Tayarisha katlesi zote hivyo hadi umalize viazi na nyama.
8.Weka mafuta katika karai yapate moto sawa sawa.
9.Chomva katlesi katika mayai uliyoyapiga sawa sawa kisha garagaza katika unga wa mkate (breadcrumbs) na uzikaange mpaka zigeuke rangi.
10.Epua weka katika karatasi ya inayokunwa mafuta (Kitchen paper) au weka katika chujio zichuje mafuta. Tayari kuliwa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

nini katomiri sisi hatuji
nini katomiri sisi hatuji jamani sadiya hapa
Assalaamu 'alaykum Tafadhali
Assalaamu 'alaykum
Tafadhali tuma swali lako kuhusu mapishi kupitia mapishi@alhidaaya.com
Hapa ni mahali pa kuweka maoni tu yanayohusu lolote usomalo hapa.
Ndugu Zako
AL HIDAAYA