Kababu Za Kuoka (Baked) Kwa Masala Ya Kutengeneza Nyumbani

Kababu Za Kuoka (Baked) Kwa Masala Ya Kutengeneza Nyumbani

Vipimo

Nyama ya kusaga - 2 Lb /1 kilo

Pilipili mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) - 2

Kotmiri ilokatwakatwa (chopped) - 1 msongo (bunch)

Chumvi - kiasi

Masala (Home Made) - 1 kijiko cha supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika bakuli, tia nyama kisha changanya vitu vyote pamoja.
  2. Tengeneza madonge ufanye shepu ya umbo la yai (oval) lakini kwa urefu zaidi kama ilivyo katika picha.
  3. Panga katika treya uliyoipata mafuta. Ukipenda weka karatasi ya jalbosi (foil). 

     4. Oka (bake) katika moto wa wastani.

     5. Karibu na kuiva, zima moto wa chini, kisha washa moto wa juu uchome (grill) kwa muda mdogo tu kwa ajili ya kababu zigeuke rangi kidogo.

     6. Epua zikiwa tayari kuliwa na saladi, mkate, au wali mweupe.

Masala Ya Kababu:

Vipimo vya Masala

Bizari nzima (cummin) - 1 kikombe cha chai

Gilgilani (corriander seeds) - 1 kikombe cha chai

Pilipili manga - ½ kikombe cha chai

Mdalasini - 5 miche

Hiliki - 10-15  chembe takriban

Uwatu (fenugreek seeds) - ¼ kikombe cha chai

Karafuu - 15-20 takriban

Majani ya bay (bay leaves) - 3

Rai (mustard seeds) - 1 kijiko cha supu

Namna ya kutayarisha Masala

  1. Safisha viungo vyote kisha viwe vikavu.
  2. Saga vyote pamoja katika mashine (Grinder) hadi iwe ni bizari ya unga.
  3. Weka katika chupa utumie unapohitajia.

Kidokezo:

Tolea na sosi ya ukwaju na nanaa katika viungo vifautavyo:
Sosi Ya Ukwaju

Chatine Ya Mtindi Na Nanaa

Share