Vitumbua Vya Kuku

VIPIMO
Kuku 3 Lb
Mayai 6
Baking Powder 1 kijiko cha chai
Pilipili boga Robo kipande
Kitunguu maji 1 kidogo
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai
Thomu na Tangawizi 1 kijiko cha supu
Chumvi ½ kijiko cha chai
Mafuta ya kuchomea
NAMNA YA KUTAYARISHA
1) Chemsha kuku mpaka awive. hakikisha umemchemsha na viungo vyote. baada ya kuwiva, toa mifupa kwa kunyambua mnofu vipande vidogo vidogo.
2) Kata kitunguu vipande vidogo vidogo
3) Kata pilipili boga (la kijani) vipande vidogo
4) Tia vitu vyote hivyo katika mashine la kusagia (Blender)
5) Tia mayai, hakikisha mayai yanafunika mchanganyiko .
6) Saga kwa muda mfupi tu.
7) Weka mchanganyiko uliosagika vizuri kwenye bakuli.
8) Tia chumvi, pilipili manga na baking powder.
9) Tayarisha chuma cha kuchomea vitumbua kwenye jiko
10) Weka mafuta kidogo
11) Choma kama unavyochoma vitumbua vya mchele.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


