Tokea Mume Ameniingilia Kinyume Na Maumbile Sina Raha Naye, Nadai Talaka Lakini Anataka Kuficha Sababu

SWALI  

Asalamu alekum,Mume wangu alinitaka na kuniingilia kwa nguvu kinyume cha maumbile.Tokea siku hiyo sikua na raha kwani alinilazimisha na wala sikutaka,alinikamata kwa nguvu.Sina mapenzi nae tena na nimemwambia anipe talaka yangu.Hataki kuniwacha na imekua ugomvi ambao umefika mpaka kwa wazee lakini ameniomba na kunishikilia nisiliseme jambo hili kwa wazee wa pande zote mbili kwa kuchelea kujiharibia heshima yake. Nimelikubali hilo lakini simuoni kama mume kwangu mapenzi hayapo tena kwangu. Nifanyeje?

Nimetengana nae miezi kazaa sasa bila kunigusa. Nasasa ni mwezi wa ramadhani bado hatusikilizani msimamo wangu ni talaka jee sina haki hii kiislamu?

 Asante nawashukuru


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalah Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Haijuzu kumuingilia mwanamke kinyume cha maumbile kwani ni katika madhambi makubwa kama ilivyothibiti kuwa

“Amelaanika anayemuingilia mwanamke kinyume cha maumbile” Abu Daawuud na Ahmad.

Pia,

“Allaah Hatomtazama mwanamume anayemuingilia mwanamke kwa nyuma” An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan.

Hivyo ni wajibu kwa Waislamu kujihadhari na jambo hili na kujiepusha na kila lililokatazwa na Allaah, na juu ya mke kutomtii mumewe katika yenye kumuasi Allaah.

Na kama ni kweli alitumia nguvu basi wewe huna kosa kwani Ummah huu umesamehewa kwa kila utacholazimishwa.

Ikiwa kweli hilo ndio tatizo basi ilikuwa hakuna haja ya wewe kutolisema mbele ya wazee ili waweze kuamua na kama kweli alikulazimisha na huna hamu naye basi ilikuwa jambo la busara kueleza ukweli wa chanzo cha ugomvi wenu jambo ambalo huenda likaweza kupelekea kuipata talaka yako, lakini unalificha kwa   kuwa utamvunjia heshima yake sasa iko wapi heshima yako kama mwanamke ambaye Uislamu unakutaka usimuachie mumeo kukuingilia kinyume cha maumbile.

Umesema, Nimetengana nae miezi kazaa sasa bila kunigusa. Nasasa ni mwezi wa Ramadhaan bado hatusikilizani msimamo wangu ni talaka jee sina haki hii kiislamu? 

Ikiwa ni hivyo basi fahamu kuwa haki unayo lakini hujaitaka, kwani kama uliweka wazi kwa wazee chanzo cha kutoelewana na mumeo kama ulivyodai kuwa amekuingilia kwa nguvu basi ungepata ukitakacho kwani ikiwa nyumba haina mapenzi wala masikilizano basi hakuna haja ya kukaa pamoja kama mume na mke; na kama kweli alikuingilia kwa nguvu basi anao uwezo wa kukugusa tena kwa nguvu kama alivyokuingia.

Pata maelezo zaidi kuhusu madhambi hayo makubwa:

Kuharamishwa Liwati

Mwenye Kufanya Maasi Ya Liwati Anaweza Kurudi Kwa Allah Kutubia?

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share