Ka-ak ( Keki Kavu Ya Kiarabu)

Ka-ak ( Keki Kavu Ya Kiarabu)

Vipimo 

Unga wa ngano - 3 Vikombe 

Unga wa atta - 2 Vikombe 

Sukari guru - 1 Kikombe cha chai 

Samli au mafuta - 1 Kikombe 

Mayai - 4 Makubwa 

Sukari nyeupe - 1 Kikombe cha chai 

Mdalasini ya unga - 2 Vijiko vya supu 

Illiki ya unga - 1 Kijiko cha supu 

Habbe soda -  1 Kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Katika bakuli kubwa, changanya pamoja unga wa ngano, unga wa atta, mdalasini, illiki na habbe soda (ukipenda isage).
  2. Yeyusha sukari guru na samli au mafuta katika moto hadi ichemke kidogo tu.
  3. Kisha mimina katika mchanganyiko wa unga huku una koroga ichanganyikane vizuri.
  4. Halafu changanya mayai pamoja na sukari nyeupe katika kibakuli, kisha mimina katika mchanganyiko na hakikisha uchanganya vizuri.
  5. Mimina kwenye sufuria au chombo cha kuchomea na huku unagandamiza gandamiza mchanganyiko kwa mkono hadi uwe umeshikamana.
  6. Kisha weka maridadi juu kwa kuchovya kwa uma.
  7. Choma kwenye oveni moto wa 350°F kwa muda wa saa 1 na robo hivi; Kisha iwache ipoe, kata vipande na itakuwa tayari kwa kuliwa na chai au kahawa.
Share