Keki Ya Rainbow

Keki Ya Rainbow

 

Vipimo

Unga - 2 gilasi

Siagi -  1 pound

Sukari -  1 pound

Mayai -  10 - 12

Baking powder -  1 kijiko cha supu

Vanila -  kiasi

Rangi mbali mbali                                                                           

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Washa oveni moto wa kiasi 350 degrees
  2. Weka siagi na sukari katika mashine ya keki, saga mpaka iwe laini
  3. Tia mayai uchanganye kwa speed ndogo. Tia vanilla changanya vizuri.
  4. Tia unga uliochanganywa na baking powder changanya vizuri
  5. Chota unga kidogo kidogo weka katika vibakuli mbali mbali utie vitone vya rangi mbali mbali
  6. Kisha changanya pamoja na mchanganyiko uliobakia, chukua kisu cha siagi uchanganye kufanya rainbow.
  7. Paka siagi katika treya ya kupikia keki.
  8. Mimina mchanganyiko upike kiasi ya nusu saa.
  9. Epua, subiri ipoe ukate upendavyo ikiwa tayari

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share