Vikeki Vidogo Vya Mviringo (Muffins) Vya Tende Na Lozi
Vipimo:
Unga 2 ½ vikombe
Sukari 1 kikombe
Chumvi 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga 1 kijiko cha chai
Baking Powder 3 vijiko vya chai
Vanilla 1 kijiko cha chai
Mayai 3
Siagi laini 350 gm
Maziwa mazito (condensed milk) 1 kikopo
Maziwa ya maji 1 ½ kikombe
Tende iliyokatwakatwa 1 ½ kikombe
Lozi zilizomenywa na kukatwakatwa slesi ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Katika bakuli, changanya vitu vikavu vyote (unga, sukari, chumvi, mdalasini, baking powder).
2. Tia katika bakuli jengine, mayai, siagi, maziwa mazito (condensed), maziwa ya maji, vanilla, na uchanganye vizuri.
3. Changanya michanganyiko miwili hiyo pamoja.
4. Changanya na tende iliyokatwa katwa .
5. Mimina mchanganyiko katika vibati vya kupikia keki au karatasi za cup cakes.
6. Nyunyizia lozi kisha uchome (Bake) katika moto wa 350°- 450° kwa muda wa nusu saa uhakikishe zimewiva.
7. Epua zikiwa tayari kuliwa.
Kidokezo:
Unaweza kufanya nusu za lozi pekee
Unaweza kutia chokoleti badala ya tende
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


