Mume Anapata Vitisho Na Matatizo Tokea Kumuoa Mke Ambaye Anasumbuliwa Na Majini

SWALI:

 

 

Asalam aleykum.naomba mnisaidie kaka yangu kaowa mke toka kaowa maisha yake yamekua na matatizo sana ikiwemo ndoto za vitisho nakadhalika na mke wake amekua na tatizo la maqjini kbl hata hajaolewa aliwahi kusumbuliwa karibu mwaka sasa pia hata mume wake akimgusa wakati mwingine hakubali na kudai kama anaona vitu vichafu hata akiwa anaswali pia anaona uchafu na kuona watu wanamuingilia tofauti na mumewe na sasa kaka yangu huyo hata kazi hana naomba ushauri wenu tufanye nini? Nitashukuru.


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu matatizo ya kaka yako na mkewe. Mwanzo ni kukuelewesha kuwa Allaah Aliyetukuka humjaribu mja Wake kwa njia tofauti ikiwemo matatizo kupitia katika ndoto. Tufahamu kuwa ndoto mbaya zinatokana na Shaytwaan na nzuri kutoka kwa Allaah Aliyetukuka. Mara nyingine vitisho katika ndoto hutokana na yale yaliyomkumba asubuhi. Ama hayo anayokumbana naye mke wake inawezekana kuwa amekumbwa na jini. 

 

 

Jambo linalotakiwa kufanywa na kaka yako ni kusoma Qur-aan na Adhkaar kwa wingi hasa Aayah za kumlinda na kukumbwa na majini. Ama kuhusu mke wake inabidi asomewe Aayah za kutolewa jini. Lau hakutakuwa na mtu mwenye uwezo wa kufanya hivyo miongoni mwenu itabidi mumpeleke kwa Shaykh atakayemfanyia dawa kwa kutumia kisomo kinachofaa cha Qur-aan (Ruqyah). Tutawahimiza musiende kwa Shaykh ambaye atatumia mambo yasiyoeleweka na ujanja ujanja au uchawi kwani hiyo itakuwa ni shirki.

 

Haya chini ni maudhui yanayohusiana na swali lako:

 

 Naingiliwa Na Majini

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Anapoweweseka Usiku Asomewe Surah Gani?

 

Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

 

Nimeambiwa Nina Jini La Kiislamu Kwa Sababu Ya Kupenda Sana Dini

 

Na Allaah Atawaafu in shaa Allaah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share