Fagi Ya Kumumunyuka Mdomoni

Fagi Ya Kumumunyuka Mdomoni

 

 

 

Vipimo

 

Maziwa mazito matamu (condensed milk)  - 2 vibati                                 

Sukari  - 1 kikombe

Samli 1 ½ kikombe

Vanilla 2 kifuniko cha chupa yake

Hiliki ilosagwa - 2 vijiko vya chai

Sinia kubwa ya bati Paka samli

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya maziwa, sukari na samli katika sufuria isiyogandisha chakula (non-stick) uweke katika moto.
  2. Koroga huku ikipikika hadi ianze kugeuka rangi na kuanza kuachana. Usiache mkono kuroga isije kufanya madonge.
  3. Tia hiliki na vanilla, endelea kuipika.
  4. Itakapogeuka rangi vizuri mimina katika sinia na haraka uitandaze kwa mwiko huku ukiuchovya katika maji na kuendelea kuitandaza hadi ikae sawa kote.
  5. Pitisha kisu kuikataka ili ikipoa iwe wepesi kuitoa vipande.

Kidokezo:

 

Kila inapozidi kupoa na kukaa ndipo fagi inakauka na kumumunyuka.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share