Sevai Kee Kheer - Tambi Za Maziwa-2 (Pakistani)

Vipimo
Siagi 2 vijiko vya supu
Tambi nyembamba
Maziwa ya ng’ombe 3 vikombe
Maziwa ya kuvukiza (evaporated milk) 2 vikombe
Zabibu kavu ½ kikombe
Sukari 3 vijiko
Lozi (zilizomenywa na kukatwa ndogondogo) ½ kikombe
Hiliki 1/3 cha chai
Vanila au arki ya rose 3 tone
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Weka siagi katika sufuria ishike moto.
2. katakata tambi vipande vitatu na uweke katika ssfuria na ukaange kwa muda hadi kuwa rangi ya hudhurungi
3. Tia maziwa na punguza moto uwe wa wastani acha ichemke
4. Kisha weka sukari, zabibu kavu, lozi, hiliki, vanilla au rose
5. Endelea kupika kwa muda wa dakika 5
6. Ongeza maziwa glass moja au mbili baridi na endelea kukoroga kwa muda kiasi
7. Epua na weka pembeni ipoe kwa muda na ongeza maziwa baridi ili ichanganyike na isigandane. Koroga na ongeza maziwa ikibidi hadi iwe nyepesi kiasi
8. Unaweza kula ikiwa moto au unaweza kuiweka katika friji ili iwe baridi.

- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
