Mishkaki Ya Kuku (Aina Ya 2)

Mishkaki Ya Kuku  (Aina Ya 2)

Vipimo 

Kuku bila mifupa - 2lb (ratili) 

Mtindi - 4 vijiko vya supu                      

Manjano - ½ kijiko cha chai                                                                                                 

Paprika - ½ kijiko cha chai  

Kuzbara (dania ya unga)  - ½ kijiko cha chai   

Kitunguu saumu (thomu) - 1 kijiko cha chai 

Tangawizi  - ½ kijiko cha chai 

Pilipili mbichi ya kusaga - ½ kijiko cha chai  

Asali - 1 kijiko cha chai 

Chumvi - kiasi 

Ndimu  - 1 

Mafuta ya zeytuni  - 2 vijiko vya supu 

Kitunguu - 1 

Kotmiri  - ¼ Kikombe  

Vijiti vya kuchomea                     

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Vijiti utaviroweka kwenye maji mapema ili visichomeke katika kuku. 
  2. Osha nyama ya kuku vizuri kisha ichuje itoke maji iwe kavu kabisa. Katakata vipande kiasi. 
  3. Changanya viungo vyote pamoja kwenye bakuli isipokuwa kitunguu na kotmiri. 
  4. Tia vipande vya kuku na roweka kutoka usiku uweke katika friji. Au roweka kwa muda wa masaa mawili takriban. 
  5. Katakata kitunguu vipande vya kiasi utunge pamoja na kuku mpaka umalize kama kwenye picha. 
  6. Choma kwenye oveni (grill) au katika jiko la mkaa hadi kuiva. 
  7. Pakuwa kwenye sahani, tupia kotmiri na vitunguu juu na tayari kwa kuliwa.

 

 

 

 

 

 

Share