Keki Ya Iyd

Keki Ya Iyd

 

Vipimo

Mayai - 5 

Unga wa keki -   1 ½ Vikombe 

Baking powder -  ½ Kijiko cha chai

Chumvi  - ¼ Kijiko cha chai 

Maji ya baridi -  ½ Kikombe 

Sukari -  1 ½ Vikombe 

Harufu ya lozi ( almond extract) -  ¼ Kijiko cha chai 

Vanilla  -  ½ Kijiko cha chai 

Malai makali (cream of tartar) -  ¾ Kijiko cha chai

  

Namna Ya kutayrisha Na Kupika 

 1. Washa oveni moto wa 325°c.
 2. Tenganisha mayai, weka viini vya mayai mbali na ute mbali.
 3. Katika bakuli kubwa, chunga pamoja unga, baking powder na chumvi na uweke kando.
 4. Piga viini vya mayai kwa mashine kwa muda wa dakika 4 hivi, kisha ongeza maji  ya baridi kidogo kidogo na huku unaendelea kupiga mpaka mchanganyiko uwe rangi ya manjano iliyoparara na kufanya povu juu.
 5. Kisha tia sukari huku unaendelea kupiga kwa dakika tatu hadi sukari iyayuke.
 6. Ongeza vanilla na harufu ya lozi kisha chunga ule mchanganyiko wa unga ndani ya mchanganyiko wa viini vya mayai, kidogo kidogo na huku unachanganya kidogo tu.
 7. Kwenye bakuli jengine, piga ute wa mayai pamoja na malai chungu (cream of tartar) mpaka iwe nzito kiasi na isikauke kwa dakika 5 hadi 6.
 8. Halafu changanya pole pole kwenye mchanganyiko wa unga.
 9. Kisha mimina kwenye chombo cha kuchomea ambacho hakikupakwa siagi.
 10. Vumbika (bake) kwenye oveni kwa muda wa saa 1.
 11. Kisha iaache ipowe na huku unaitayarishia malai (whip cream frosting).    

Malai Ya Vanilla (Kupaka na Kupambia Keki) 

Vipimo: 

Siagi laini isiyo na chumvi -  ½ kikombe

Sukari ya podari (Icing Sugar) -  4 vikombe

Maziwa -   1/3 kikombe

Vanilla - kijiko cha chai 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 1. Katika bakuli, tia siagi na isage na kuichanganya hadi iwe laini  
 2. Tia icing sugar, maziwa na vanilla uchanganye zaidi vizuri hadi iwe laini kabisa kama malai.  
 3. Punguza kidogo utie katika kidude cha kupambia (icing nozzle) kilichokuwa na design   
 4. Punguza pia kidogo sana kwa ajili ya  kutia rangi  ya kupambia au kuandikia.  
 5. Paka malai juu ya keki kwa kutumia kisu kipana kama cha siagi au mwiko wake hasa, huku unachomva katika maji. Tandaza vizuri kote.  
 6. Pambia pembezoni mwa keki kwa kukamua kidude cha icing (icing nozzle) .  
 7. Tumia malai ya rangi kwa ajili ya kupamba na kuandikia upendavyo.

 

 

 

 

 

 

Share