Keki Ya Mirabaraba Ya Malai (Cream Checks Cake)

Keki Ya Mirabaraba Ya Malai (Cream Checks Cake)

                                                                                                                    

Vipimo

Keki ya pauni (pound cake) yatayari -  2 (moja ya vanilla na moja ya chokoleti)

Malai ya jibini (cream cheese) - 1 Pakiti

Malai ya karameli (cream caramel) - 1 Pakiti

Mchapo wa malai (whip cream) - 1 Pakiti

Malai ya Nestle (Nestle cream) - 1 Pakiti

Sukari - 1 Kikombe

Shira ya chokoleti (ukipenda) - Kiasi

Karatasi la plastiki (wax paper)

Namna ya kutayarisha

1.  Tayarisha treya kwa kutandaza karatasi la plastiki

2.  Kata keki vipande kwa umbo la mraba, kisha panga kwenye treya kama ilivyo katika picha

3.  Kisha changanya vipimo viliyobakia na mimina juu ya keki na unyunyiziye shira ya chokoleti

 

4.  Halafu pangilia vipande vya keki tena juu ya mchanganyiko wa malai 

5.  Kisha weka ndani ya freezer kwa muda wa saa moja hivi.

6.  Kabla ya kuanda, weka treya nyingine kubwa juu ya keki na upendue keki upande wa pili, kisha toa karatasi na itakuwa tayari kwa kuliwa. 

Kidokezo:

Badala ya kuweka mchanganyiko wa malai katikati ya keki, unaweza kutia ice creamu uipendayo, kisha weka keki kwenye freezer kwa muda wa masaa 2 kabla ya kuipakua.

 

  

Share