Amempeleka Mke Nchi Za Kimagharibi Anakopata Matumizi Ya Serikali - Kisha Kamtelekeza Na Kudai Kuwa Ameshatimiza Wajib Wake

 

SWALI:

 

Assalaamu alaykum warahmatu llahi wabarakaatu. mimi nina maswali yangu naomba ufafanuzi kidogo inshaallah. Mume wangu kanileta ulaya halafu yeye akarudi afrika akaoa, mkewe wa afrika anampa mahitaji yake yote, mimi nikamwambia wewe umeoa na mkeo unampa mahitaji yake mbona mimi hunipi, nalishwa, navishwa, napewa pa kukaa na serikali? akanijibu kua, yeye ndo alonileta ulaya kwa hiyo mimi nikipewa mahitaji yangu na serikali ni kua yeye ndo alofanya vile kwa sababu yeye ndo alonileta kwa pesa yake, na mahitaji ambayo napewa yeye ndo anaenipa kwa sababu ndo alonileta, na anasema kwamba kwani ukifanya biashara halafu ukipata faida ile faida inakua siyo? Kwa hiyo madamu yeye kanileta ile kulipwa ndio faida yenyewe ile, naomba mnijibu ndivyo sheria inavyosema?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kupelekwa kwako Ulaya kisha kutelekezwa. Naona dada yetu yapo mambo ambao umeyaacha hapo katikati ambayo yangetusaidia kuweza kukujibu kwa njia ambayo ni nzuri zaidi.

 

Hata hivyo, tutajaribu kukujibu kwa ujumba tunadhania kuwa utapata nasaha muwafaka katika hilo. Mwanzo ya yote kwako kupelekwa Ulaya na mumeo kulikuwa na mapatano ya aina yoyote yale? Kwa mfano mimi nakupeleka Ulaya, serikali itakupatia kwa niaba yangu pesa zako zote za matumizi. Na pia hizo pesa unazopata na matumizi unakwenda kuzichukua kwa jina la mumeo au kwa jina lako. Ikiwa kulikuwa na mapatano kuwa mume atakupeleka Ulaya na huko utakuwa unapatiwa pesa na serikali kwa hiyo hutanidai kitu mapatano hayo yatakuwa hivyo. Sababu yake ni kuwa Waislamu wako katika ahadi waliyopeana.

 

Ikiwa kupelekwa kwako Ulaya unapata marupurupu (pesa) ambazo ni za mumeo itakuwa ni kama yeye aliyekupa kwa kuwa ni zake naye ametoa maagizo upewe wewe. Kwa njia hiyo hutaweza kutaka masurufu mengine, jambo ambalo utahitajia kisheria ni lazima mumeo akawe siku baina yako na yule mke wa Afrika. Na lau itakuwa yeye amekuandikisha wewe uwe utapata pesa hiyo itakuwa ni ihsani kutoka kwake lakini masurufu yako itabidi atume tena kando kama mume wako ambaye ana majukumu ya kufanya hivyo kisheria.

 

Kukuleta ni mbali na majukumu nayo ni mbali ambayo yanahitajiwa kutimizwa kwa njia iliyo bora.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share