Kumwita Shekhe Nyumbani Asome Khitma Inafaa?

 

Kumwita Shekhe Nyumbani Asome Khitma Inafaa?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Kumwita shekhe kusoma hitma nyumbani kwako na kumlipa je hiyo inaruhusiwa? Naomba mnisaidie kwa maswali hayo tafadhali.

 

shukrani.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Haikupatikana kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) wala waliomfuata katika watangu wema ambao walikuwa wanakwenda majumbani kusoma khitmah.

 

Khitmah mwanzo ni kuhitimisha Qur-aan na linalofaa ni wewe mwenyewe kusoma Qur-aan kuanzia mwanzo mpaka umalize, yaani kuanzia Suwrah Al-Faatihah hadi Suwrah Al-Naas. Unapomaliza msahafu wote ndio inakuwa umehitimisha Qur-aan. Mara zote mwanzo tunapowaita mashaykh kufanya hivyo huwa hatuhitimishi bali ni danganya toto.

 

Qur-aan inatakiwa uisome mwenyewe, jaribu kuifahamu na ufuate maagizo yaliyo ndani yake.

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

 

Kumsomea Khitmah Maiti, Kumchinjia Na Kumuombea Duaa Kwa Pamoja

 

Khitmah Kutokufaa Na Madhara Yake

 

Kusoma Khitma Inafaa?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share