Amemtamkia Mke Aliye Aasi Anakufuru Dini Yake Talaka Tatu Mbali Mbali Kisha Bado Anamtaka. Mke Wa Pili Anataka Kuachwa

SWALI:

 

 

HILI..NIMEJARIBU KUANDIKA KTK SEHEMU YATUMA MASWALI ILA INAGOMA KWA KUWA MAELEZO NI MENGI

 

KUNA MTU AMBAE ALIOA MWAKA 2003, MKE WA PILI 2007 NA MPAKA SASA AMESHAMTAMKIA MKEWE WA KWANZA TALAKA TATU TOKA 2003 -2009, ILA KUNA WATU, AKIWEMO NA YEYE HUYO MUME SASA WANADAI KUWA TALAKA HIZO HAZIKUBALIKI ISIPO KUWA MOJA TU KATI YA HIZO TATU HIVYO ANATAKA KUMRUDIA ALIEKUWA MKEWE.

 

MOJA- (2003)

 

ALIMKAMATA MKEWE AKIWA NA MAWASILIANO YA KIMAPENZI NA MWANAMUME MWINGINE ILA HAKUWAHI KULALA NA MPENZI WAKE HUYO. BADA YA KULETA KESI KWA WAZAZI WA MWANAMKE AMBAO WAO DINI NI KAMA PAMBO NA WANAPINGA VINGI KTK UISLAM NA MBELE ZA WATU WAPO RADHI HATA KUSEMA WAO SI WAISLAM WAKAMJIBU KUWA YEYE MUME YUKO BUSY NA KAZI ANATEGEMEA MTOTO WAO AISHI VIPI BILA MWENZA..KUTOKANA NA KAULI ZAO HIZO AKAMPA HASIRA AKAAMUA KUMPA TALAKA.. KISHA AkAMREJEA.. MKE WAKE BADA YA SIKU CHACHE..MKE HUYO PIA ANAPINGA VITU VIGI SANA KTK DINI HATA HIJAB HATAKI KUVAA ANASEMA  KWA NINI MUNGU ALITUUMBA WAZURI KISHA ANASEMA TUJIFUNIKE, PIA AKASEMA YEYE HAWEZI KUJISITIRI MAADAM BABA YAKE MZAZI KAMWAMBIA ASIFANYE HIVYO..UGOMVI WAO UKAENDELEA AKAMWAMBIA MUMEWE AOE MKE ANAEFATA DINI MANA YEYE HAWEZI KUFATA DINI MPAKA ATAKAPOFIKA MIAKA 50..

 

YA PILI (April 2008)

MUME AKAOA MKE ANAEFATA DINI..MWANAMKE WIVU UKAMUIJIA AKAMWAMBIA MUMEWE AMUACHE MKE WA PILI, NA ASIFUGE NDEVU TENA AZIKATE KWA KUBADILISHANA YEYE AVAE HIJAB NA AANZE KUFATA DINI, MUME AKAMWAMBIA ATAACHA KUFUGA NDEVU YEYE AVAE HIJAB, WALIPOSHINDANA KWA HILO MKE AKAMWAMBIA MUME KUWA ATAKWENDA KUMSHITAKI AFUNGWE JELA MANA SHARIA YA NCHI HAIRUHUSU MUME KUWA NA WAKE WAWILI,.ALIPOTISHIA HIVYO MUME AKAAMUA KUMPA TALAKA KWA NJIA YA SIMU AKIWA ANAENDA KAZINI ASUBUHI..BADA YA SIKU CHACHE MUME AKAENDA KUMRUDIA TENA.

 

TALAKA YA TATU (April 2009)

MAISHA YA WATU HAWA YAKAENDELEA KUWA YA UGOMVI MKUBWA BAINA YAO, UGOMVI HUO NI KUWA YEYE HATAKI KUFATA MAAGIZO YA QUR-AN MPAKA MKE MDOGO AACHWE, NA ARUDISHWE KWAO,, AKAWA NA MSIMAMO AKIPEWA TALAKA MKE WA PILI AMBAYE TAYARI ANAMTOTO YEYE ANAWEZA KUJIFIKIRIA KUVAA HIJABU..SIO KUWA ATANZA KUVAA  "ANAWEZA KUJIFIKIRIA" ILA KWA KUWA YUPO ANAEMRIDHISHA MUMEWE KWA MAMBO YA DINI YEYE HAWEZI KUFANYA HAYO..KWA KUWA WAZAZI WAKE WAPO KINYUME NA DINI NA YEYE ANASIKILIZA WAZAZI WAKE WALIPOJUA KUWA MKWE WAO ANAMKE MWINGINE WAKAINGILIA KATI NA KUMFUKUZA HUYO BWANA NYUMBANI KWAO USIKU WA MANANE..BWANA AKAMULIZA MKEWE KAMA ATAFATANA NAE AKAKATAA MBELE YA WAZEE WAKE, AKARUDI KWA MKE MDOGO KWA SIKU 3 KILA SIKU ANAMULIZA MKEWE UNATAKA KUNIFATA ANASEMA "SIWEZI KUKUFATA NATAKA TALAKA"..WAKAAMUA KWENDA MAHAKAMANI NA HII IKIWA NI MARA YA PILI KWENDA AJILI YA TALAKA YA TATU..MARA YA KWANZA WALIENDA WAKAGAIRI KUACHANA, HII YA PILI WAKAENDA WAKAAMBIWA WATAITWA NA QADHI BADA YA MWEZI..WALIPOFIKA NYUMBANI AKAFICHA DOCUMENTS ZA WATOTO NA KUDAI APEWE TALAKA YAKE, MUME WAKE  KWA HASIRA AKAAMUA KUMPA TALAKA BILA KUSUBIRIA SIKU WATAKAYO ITWA AMBAPO WALIKUWA WAITWE BADA YA MWEZI, MWANAMKE AKAENDA KUMWITA MAMA YAKE AWE SHAHIDI, WALIPOKUJA MUME AKAKATAA KURUDIA KUITAMKA TALAKA...AKAFUNGA MIZIGO YAKE NA KUONDOKA.

 

TOKA WAACHANE SASA UMEPITA MWEZI NA SIKU ISHIRINI, AKAONANA NA WATU WAKAMWAMBIA KUWA TALAKA YA KWANZA NA YA TATU HAZIKUBALIKI KWA KUWA ZILIKUWA NA UGOMVI KABLA NA ALIKUWA NA HASIRA..CHAA AJABU NI KUWA VIPI WATU WAMEFUNGA SAFARI YA ZAIDI YA NUSU SAA KWENDA MAHAKAMANI MARA 2 KUACHANA KISHA WAKAAMUA KUACHANIA NYUMBANI ISEMEKANE SIO TALAKA? INAMAANA HATA INGETAMKWA MAHAKANAI ILIKUWA SIO TALAKA MANA WALITOKA NYUMBANI KWA UGOMVI??

SASA HUYO MUME BADA YA KUAMBIWA HIVYO KAANZISHA MAWASILIANO NA ALIEKUWA MKEWE NA ANAMWITA MKEWE SIO "X-WIFE"

 

MKE MDOGO ANATAKA KUJUA MANA ANAIMANI KUWA HIZO NI TALAKA TATU ZISHATIMIA, ANADAI IKIWA WATARUDIANA YEYE ANAOMBA KUTOKA KTK NDOA HII MANA ITAKUWA ANAMSUPPORT MUME WAKE KUFANYA ZINAA NA ALIEKUWA MKE WAKE KWA MANA WALISHA ACHANA..KAMWAMBIA MUMEWE AOE MKE MWINGINE NA YUPO TAYARI KUMTAFTIA KAMA ANATAKA WAKE WAWILI AU ZAIDI LAKNI SI KUMRUDIA YULE MUME YE ANAMTAKA YULE  HATA KAMA HAFATI DINI KAAMBIWA ETI KILA MTU NA DHAMBI ZAKE HAWEZI SIKU YA KIAMA AKAAMBIWA KWA NINI MKEWE ALIKUWA ANATEMBEA UCHI NA HATA KWENDA UFUKWENI NA VICHUPI TU WAKATI WA SUMMER ANAENDA UFUKWENI NA NGUO ZANDANI TU..NA ANADAI YEYE NA BABA YAKE KUWA AKIJISITIRI NA KUFATA DINI HATOPATA WATEJA KAZINI YEYE NI MWANASHERIA..PIA KUSOMESHA WATOTO WAKE QUR-ANA ANSEMA BADO WADOGO ITAWACHANGANYA, WAKATI MTOTO WA KWANZA ANA MIAKA 8 ANAENDA 9, NA MDOGO ANAMIAKA 5, ILA YUPO RADHI KUPOTEZA PESA  YOYOTE KUWALETEA MWALIMU WAKUWAFUNDISHA KUOGELEA NYUMBANI, KUNUNUA VITABU VYA HADIHTI ZA KIDUNIA, KUWANUNULIA KASETI ZA KILA TOLEO LA KARTOON, KUPIGA PIANO, NA KUWALIPIA SHULE ZA KUCHEZA BALLET DANCES..YANI MKE HUYO HANA CHEMBE YA DINI HATA KIDOGO YEYE NA FAMILI YAKE NA MUME TOKA MWANZO HANA SAUTI HATA KIDOGO JUU YA MKEWE WALA WATOTO, NA HATA AKITOKA NA NGUO ZA NDANI MUME HANA UWEZO WA KUMZUI, ILA YUPO RADHI KUMCHUKUA TENA JAPO KUWA KESHA TAMKA TALAKA MARA TATU ILA KWA KUWA KAAMBIWA HASIJUZU BASI ANATAKA KUTUMIA FURSA HIYO KUMRUDIA..KISINGIZIO ETI WATOTO AWEZE KUONA WATOTO WAKE MANA TOKEA AHAME NYUMBA HIYO WANAMPA MASHARTI YA KUOANA WATOTO

 

TUNAOMBA USHAURI WENU HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WAJUE KAMA WAPO SAHIHI AU MKE HUYU MDOGO AONDOKE.

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu talaka na ujasiri wa mke kufanya maasiya. Hakika tumesoma habari hii kwa masikitiko makubwa sana kuona jinsi Ummah ambao ulikuwa unatakiwa kuwa bora unavyohangaika na mambo ya Kimagharibi mpaka kuacha desturi na ada zao wakihimzwa watoto na wazazi wao.

 

Awali ya yote ni kuwa talaka inapotolewa kwa ajili ya hasira ya mume basi imepita. Talaka ni jambo halina mzaha, mzaha wake ni kweli na ukweli wake ni ukweli. Kwa hiyo, mume akiwa ana hasira akatoa talaka, talaka yenyewe imepita na kwa sababu ametoa talaka tatu, watu hao wawili hawezi kurudiana mpaka mke aolewe na mume mwingine, wakutane kimwili kisha waachane kawaida ndio mume wa kwanza ataweza kumrudia mkewe huyo.

 

Tunastaajau kusikia kuwa mume anafunga ndefu na alikuwa anafanya juhudi kutafuta mke anayefuata Dini akampa kisha bado akawa anampenda na kutaka kumrudia mwanamke ambaye ni aasi na maneno hayo mliyosema kama ni uhakika basi mwanamke huyo si Muislamu kamwe. Huyu anatakiwa ashauriwe kwani katika Uislamu, mume ndiye mwenye mamlaka ya nyumba na ikiwa mume hatoweza kutekeleza jukumu hilo atakwenda mahali pabaya kwani moto ndio utakuwa makazi yake. Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) anatuambia kuwa watu watatu hawatosikia hata harufu ya peponi. Mmoja wao ni Dayyuth. Dayyuth ni mwanamme ambaye hajali mkewe anafanya nini wala hashughuliki.

 

Nasaha ambayo tungempa mke wa pili ni kuwa ajaribu kuzungumza na mumewe kwa njia ya busara, nzuri na utaratibu kuhusu kosa kubwa analofanya. Ikiwa mume atasikia na kujirekebisha itakuwa sawa, ikwia hatosikia basi huo ni munkar ambao Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) ametuagizia kuuondosha kwa mkono, ulimi au kuchukia katika nafsi. Jambo ambalo unatakiwa kufanya ni kwenda kwa Qadhi na kushitaki kuhusu tendo hilo la mumeo, na ikiwa ataendlea itabidi uombe talaka kwa maksoa ya mume umuache yeye na uzinzi wake.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share