Mke Kupashwa Habari Kuhsu Uzinzi wa Mumewe Na Kaapishwa Kuwa Asitaje Aliyempasha

SWALI:

 

Asalaaam aleikum warahmatulrahi wabarakatah. NINA SWALI NATAKA JIBU LAKE; Mke wa mtu kaambiwa na mtu ambaye hataki kumtaja kwa sababu huyo aliesema maneno hayo kamuapisha kuwa asimwabie mtu yoyote na maneno aliyomwambia ni kuwa mume wake ana mwanamke mwingine wa nje (HAWARA) na anatembea nae na kuwa mumewe anafanya mambo mabaya ya qaumu lut na huyo mwanamke. Mke kuambiwa khabari hizo kamkasirikiya sana mume wake wa miaka 30 kafikia hatua ya kudai talaka, Mume kamuapuia kua khabari hizo ni za urongo na fitina tu na kamtaka mkewe amtaje huyo muongo lakini mke hataki kumtaja eti kaapishwa asimtaje. SWALA je akimtaja atadhurika? (kwa kiapo alichokula) na nini hukumu ya huyo mke kusikiza fitina hizo na kutoamini maneno ya mumewe?

 

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mke kupashwa habari na mtu kuhusu uzinzi na ubaya wa mumewe. Hakika tumejirudisha nyuma sana kwa kuwa na mambo kama haya yanayoendlea katika jamii yetu ambayo ni jamii ya kutakia mema na undugu baina yao. Muislamu mwema ni yule ambaye anaziba makosa ya watu na huku anajaribu kuwanasihi ili waache maasiya hayo. Muislamu anatakiwa zaidi awe ni mwenye kunasihi na sio kufedhehi mwingine kwa njia yoyote ile.

 

Na jameni ndugu Waislamu, fitna hizi zimekithiri na sasa zimeelekea kuvunja majumba ya watu walioishi kwa muda mrefu, miaka thelathini kwa tuhma ambazo hazina msingi wa aina yoyote. Nasaha kwa ndugu zetu ni kuwa ikiwa mtu amekuja kukupasha habari ya mtu yeyote yule inatakiwa umwambie kuwa ngojea nimuite mwenyewe. Kufanya hivyo ni kuweza kupima ukweli wake. Ikiwa ni kweli atakuwa yuko tayari kwa hilo lakini akiwa si mkweli atakuwa ni mwenye kupapatika na kukwambia achana ya suala hilo, basi yaishe na mengineyo mengi. Mtu akikuambia hivyo basi tahadhari naye sana na jaribu kumweuka kwani si mwema kwako.

 

Kwa sasa cha kufanya ni mambo mawili:

 

  1. Mwambie yule aliyekuambia kwamba nataka kutatua tatizo hili ambalo umeniletea kwa tunakuta mimi, wewe na mume wangu.

 

 

  1. Mwamini mumeo na usahau fitna za watu wenye kutaka kuharibu nyumba za watu.

 

Na jambo ambalo ni jema kwa mama huyo kufanya ni kutengeneza uhusiano wake na mumewe na aepukane na huyo aliyekuja kutia fitna na kusahau yaliyopita wala usiwe ni mwenye kulitaja tena.

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate makala muhimu kuhusu fitna kama hii:

 

Madhara Ya An-Namiymah (Kufitinisha Baina Ya Watu Wachukiane) 1 Maana, Hukumu Na Adhabu Zake

 

Madhara Ya An-Namiymah (Kufitinisha Baina Ya Watu Wachukiane) 2 - Sababu za Kufitinisha, Sifa Za Mfitinishaji

 

 

 

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Awaondolee mahasidi na vitimbi vya wafitinifu.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share