Anataka Tafsiri Ya Kiswahili Ya Mawlid Barzanji Ili Ajue Nini Hasa Kimeandikwa Ndani Yake.

 

SWALI:

Assalam laykum

tumekua tukisma mara nyingi makala zinazokataza mawlid na zinazo kubali mawlid na kuzusha mijadala mingi sehemu mbalimbali na wengi wa wanaotoa mada hizi huwa na hoja zao japo nyengine si za msingi, kwa hiyo ombi langu kwenu naomba mtutilie tafsiri ya kiswahili ya mawlid al barzanji ili tupate nafasi ya kujua nini hassa kimeandikwa ndani ya kitabu hichi. Natanguliza shukran.

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu tafsiyr ya Barzanji.

Hakika inatosha kwa Muislamu kujua kuwa Mawlid ni jambo la uzushi na lisilomsaidia Muislamu katika Diyn yake wala kumpatia pepo yake.

Ikiwa ni  hivyo basi, hakuna maana yoyote wala haja ya Muislamu kutaka kujua tafsiyr ya hivyo vijitabu vinavyotumika kusomea Mawlid.

 

Lakini ikiwa unaona ni muhimu kwako kujua ili uweze kuwatanabahisha wengine na waache uzushi huo, basi, kuna kitabu cha Shaykh Abdullah Saleh Farsy ambaye alikuwa ni Qaadhi wa Zanzibar na Kenya, yeye ametafsiri hiyo Barzanji na katanabahisha yale makosa yaliyomo humo ndani. Bonyeza kiungo kifuatacho ukipate maelezo yake.

Makosa Yaliyomo Katika Mawlid Ya Barzanjiy, Burdaa, Nuwn, Sumtudurrar, Dalaailul Khayraat, Du'aa Ya Wasiylah Na Mawlid Mengine -- Uzushi na Maovu

 

Viungo vifuatavyo pia vinatoa mafunzo kuhusu uzushi huo.  :

Zijue Sababu Za Kumfanya Muislam Asisherehekee Maulidi

Hoja Za Wanaosherehekea Mawlid Na Majibu Yake

Mawlid Ni Bid'ah Na Vigawanyo Vya Bid'ah Pia Ni Bid'ah

Hukumu Ya Kusherehekea Kuzaliwa Kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share