Surah Ziloteremka Makkah Na Za Madiynah

SWALI:

 

Asalamu alaykum warahmatu LLwah wa barakatu. Mimi napenda kuuliza suali. Kuna sura ngapi zilizo teremka Maka na sura ngapi zilizo teremshwa Madinaa? Naomba nifahamishwe. Ahsante

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu idadi ya Surah zilizoteremshwa Makkah na zile za Madiynah.

 

 

Hakika katika hili Wanachuoni wametofautiana na kupatikana kauli tatu. Nazo ni kama zifuatazo:

 

 

 

 

Kauli

Makkah

Madiynah

1. Ya kwanza

86

28

2. Ya pili

87

27

3. Ya tatu

88

26

 

 

Tofauti hizi zimetokana na baadhi ya Surah ambazo Wanachuoni wengine wameziona na kuziorodhesha kuwa zimeteremshwa Makkah na wengine kuwa ni za Madiynah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share