Kujikinga Na Shaytwaani Katikati Ya Surah Unaposoma Qur-aan

SWALI:

 Je, ikiwa unasoma Qur-aan na umeanza katikati ya sura inafaa kusema A'udhu Billahi Mina-Shaytaanir-Rajiym 

 

 JIBU

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Ni sawa kabisa kuanza kusoma Qur-aan kwa A'udhu Billahi Mina-Shaytaanir-Rajiym   ikiwa ni  katikati  ya sura kwani tumeamrishwa kufanya hivyo mtu anapoanza kusoma Qur-aani kama katika aya hii :

)) فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ ((

 ((Na ukisoma Qur-aan muombe Allaah  Akulinde na shaytwaan maluuni))   [An-Nahl: 98]

Unaweza pia kuongezea na Bismillahir-Rahmaanir-Rahiym hata kama ni katikati ya Surah.  Na kama ni mwanzo wa Surah basi  uanze na A'udhu Billaahi Mina-shaytwaanir-Rajiym Bismillaahir-Rahmaanir-Rahiym  isipokuwa Suratu-Tawbah ambayo inaanzwa kwa A'udhu Billaahi Mina-shaytwaanir-Rajiym    bila ya kusema Bismillaahir-Rahmaanir-Rahiym.

 

Wallaahu A'aalam

 

 

Share