Mke Wake Ana Ukimwi Je Aendelee Kuishi Naye?

SWALI:

Nimewahi kuuliza lakini sikupata jibu niswali ligumu na ninapendelea kupata jibu, ni mtuu anaishi na mkee wake alafu mkee wake kapata ujauzito alafu mkee kapimwa kakutana ana umwa ukimwi na mee ana sasa itakuwa vipi kuusu kuu ishi pamoja napendelea kupata jibu juu madocta wanasema kama munaweza kuishi pamoja na ukaendelea kumuingilia

 

 


JIBU:

 Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Katika Uislamu mwanamume anaruhusiwa kutoa talaka ikiwa mkewe ana maradhi hatari. Pia mke anaruhusiwa kuomba talaka ikiwa mumewe ana maradhi ya hatari kwa sababu sheria yetu ya Kiislamu haipendelei kusababishiana madhara.

Amesema  Mtume  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa salam)  ((Haifai kudhuru wala kulipana madhara)) [Hadiyth Hasan iliyopokewa na Ibn Maajah, Maalik na ad-Daaraqutniy]

Maradhi ambayo mwanamke anaruhusiwa kuomba talaka ni matano:

1-   Uwendawazimu usiopona kabisa

2-   Ukoma

3-   Mbalanga

4-   Mwanamume ambaye hawezi kufanya kabisa tendo la ndoa

5-   Mwanamume mwenye ugonjwa wa pongwa (kukatika kipande sehemu ya uume wake)

Ikiwa mwanaume hana uwezo wa tendo la ndoa atapewa muda wa mwaka mmoja wa kujitibia ikishindikana mke anapewa khiyari ya kuchagua kati ya kubakia katika maisha ya ndoa yale au kuachana na maisha ya ndoa na mume yule.

Ama maradhi haya ya ukimwi pia mke au mume kila mmoja ana khiyari kati ya mambo mawili tuliyoyataja.

Kadhalika mume atakuwa na khiyari ya kutoa talaka ikiwa mkewe atakuwa na moja ya maradhi yafuatayo:

1-   Uwenda wazimu usiopona

2-   Ukoma

3-   Mbalanga

4-   Kuota nyama sehemu ya siri

5-   Kuota kifupa sehemu ya siri ambayo humuondolea raha ya maisha ya tendo la ndoa pia humsababishia maumivu makali.

Hivyo chukulia kwa mfano huo kila ugonjwa ambao ni hatari katika maisha ya mwanaadamu.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share