017 - Al-Israa

 

  الإِسْرَاء

 

Al-Israa: 017

 

(Imeteremka Makkah)

 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١﴾

1. Utakasifu ni wa Ambaye Amemsafirisha usiku Mja Wake kutoka Al-Masjid Al-Haraam mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumebariki pembezoni mwake, ili Tumuonyeshe baadhi ya Ishara Zetu. Hakika Yeye (Allaah) Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.

 

 

 

وَآتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُوا مِن دُونِي وَكِيلًا ﴿٢﴾

2. Na Tumempa Muwsaa Kitabu na Tukakifanya mwongozo kwa wana wa Israaiyl kwamba: Msimfanye yeyote badala Yangu kuwa ni mtegemewa.

 

 

 

ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَبْدًا شَكُورًا ﴿٣﴾

3. Enyi kizazi cha ambao Tuliwabeba pamoja na Nuwh (katika jahazi)! Hakika yeye alikuwa mja mwingi wa shukurani.  

 

 

 

وَقَضَيْنَا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا ﴿٤﴾

4. Na Tuliwajulisha wana wa Israaiyl katika Kitabu kwamba: Bila shaka mtafanya ufisadi katika ardhi mara mbili, na kwa hakika mtapanda kiburi cha dhulma na kutakabari kukubwa.

 

 

 

فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ ۚ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا ﴿٥﴾

5. Basi utakapowadia wakati wa mara ya kwanza yao (fisadi mbili) Tutakutumieni Waja Wetu wenye nguvu kali za kupigana vita, waingie kusaka nyumba kwa nyumba, na hii ni ahadi, lazima itekelezwe.

 

 

 

ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ الْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ وَأَمْدَدْنَاكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَجَعَلْنَاكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا ﴿٦﴾

6. Kisha Tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao, na Tukakuongezeeni mali na wana, na Tukakufanyeni wengi zaidi kwa idadi na nguvu.

 

 

 

إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ ۖ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا ۚ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيرًا ﴿٧﴾

7. (Na Tukasema): Mkifanya ihsaan basi mnajifanyia ihsaan kwa ajili ya nafsi zenu wenyewe, na mkifanya uovu, basi hasara ni juu yake. Na utakapowadia wakati wa mara ya pili, (Tutakutumieni tena maadui) ili wadhalilishe nyuso zenu, na ili waingie Msikitini kama walivyouingia mara ya kwanza, na ili wateketeze kila walichokiteka kwa mateketezo makubwa.

 

 

 

عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يَرْحَمَكُمْ ۚ وَإِنْ عُدتُّمْ عُدْنَا ۘ وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ حَصِيرًا ﴿٨﴾

8. Asaa Rabb wenu Akakurehemuni. Na mkirudi (kwenye ufisadi na dhulma), Nasi Tutarudi (kukuadhibuni). Na Tumeifanya Jahannam kwa makafiri kuwa ni gereza.

 

 

 

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا ﴿٩﴾

9. Hakika hii Qur-aan inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa.

 

 

 

وَأَنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٠﴾

10. Na kwamba wale wasioamini Aakhirah Tumewaandalia adhabu iumizayo. 

 

 

 

وَيَدْعُ الْإِنسَانُ بِالشَّرِّ دُعَاءَهُ بِالْخَيْرِ ۖ وَكَانَ الْإِنسَانُ عَجُولًا ﴿١١﴾

11. Na binaadamu huomba shari kama vile aombavyo kheri. Na binaadamu ni mwenye pupa mno.

 

 

 

وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ آيَتَيْنِ ۖ فَمَحَوْنَا آيَةَ اللَّيْلِ وَجَعَلْنَا آيَةَ النَّهَارِ مُبْصِرَةً لِّتَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ وَلِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ وَكُلَّ شَيْءٍ فَصَّلْنَاهُ تَفْصِيلًا ﴿١٢﴾

12. Na Tumejaalia usiku na mchana kuwa ni alama mbili. Tukafuta alama ya usiku na Tukajaalia alama ya mchana kuwa ni ya mwangaza ili mtafute Fadhila kutoka kwa Rabb wenu, na ili mjue idadi ya miaka na hesabu (nyinginezo). Na kila kitu Tumekifasili tafsili ya waziwazi kabisa.

 

 

 

وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ ۖ وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنشُورًا ﴿١٣﴾

13. Na kila binaadamu Tumemuambatanishia ‘amali zake shingoni mwake. Na Tutamtolea Siku ya Qiyaamah kitabu akikute kimekunjuliwa.[1]

 

 

 

اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا ﴿١٤﴾

14. (Ataambiwa): Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosheleza leo kukuhesabu.

 

 

 

مَّنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۗ وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا ﴿١٥﴾

15. Anayehidika, basi anahidika kwa manufaa ya nafsi yake. Na anayepotoka, basi anapotoka kwa khasara yake. Na wala mbebaji (wa dhambi) hatobeba mzigo wa mwengine. Na Hatukuwa Wenye Kuadhibu mpaka Tupeleke Rasuli.

 

 

 

وَإِذَا أَرَدْنَا أَن نُّهْلِكَ قَرْيَةً أَمَرْنَا مُتْرَفِيهَا فَفَسَقُوا فِيهَا فَحَقَّ عَلَيْهَا الْقَوْلُ فَدَمَّرْنَاهَا تَدْمِيرًا ﴿١٦﴾

16. Na Tunapotaka kuangamiza mji, Tunawaamrisha wastareheshwa wake wa anasa za dunia, nao wakaendelea kufanya ufasiki humo, na hapo ikastahiki juu yake kauli (ya adhabu), kisha hapo Tunaudamirisha kwa mateketezo makubwa.

 

 

 

وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِنَ الْقُرُونِ مِن بَعْدِ نُوحٍ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا ﴿١٧﴾

17. Ni nyumati nyingi sana Tumeziangamiza baada ya Nuwh. Na Rabb wako Anatosheleza kabisa Kuwa Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri, Mwenye Kuona dhambi za Waja Wake. 

 

 

 

مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا ﴿١٨﴾

18. Yeyote anayetaka (starehe za dunia) ipitayo upesi upesi Tunamharakizia humo Tuyatakayo, kwa Tumtakaye. Kisha Tutamjaalia Jahannam aingie na kuungua hali ya kuwa mwenye kushutumiwa na kufukuziliwa mbali. 

 

 

 

وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا ﴿١٩﴾

19. Na anayetaka Aakhirah na akaifanyia juhudi inayostahiki kufanyiwa, naye ni Muumin, basi hao juhudi zao ni za kushukuriwa. 

 

 

 

 

كُلًّا نُّمِدُّ هَـٰؤُلَاءِ وَهَـٰؤُلَاءِ مِنْ عَطَاءِ رَبِّكَ ۚ وَمَا كَانَ عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا ﴿٢٠﴾

20.  Wote hao Tunawakunjulia - hawa na hao - katika Hiba za Rabb wako. Na hazikuwa Hiba za Rabb wako zenye kuzuiliwa.

 

 

 

انظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ وَلَلْآخِرَةُ أَكْبَرُ دَرَجَاتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلًا ﴿٢١﴾

21. Tazama vipi Tulivyowafadhilisha baadhi yao juu ya wengineo. Na bila shaka Aakhirah ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi.

 

 

 

لَّا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَّخْذُولًا ﴿٢٢﴾

22. Usifanye pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine, ukaja kushutumiwa na kutelekezwa mbali (motoni). 

 

 

 

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾

23. Na Rabb wako Ameamuru kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff![2] Na wala usiwakemee, na waambie maneno ya heshima.

 

 

 

وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

24. Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme: Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni.

 

 

 

رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمْ ۚ إِن تَكُونُوا صَالِحِينَ فَإِنَّهُ كَانَ لِلْأَوَّابِينَ غَفُورًا ﴿٢٥﴾

25. Rabb wenu Anajua zaidi yaliyomo katika nafsi zenu. Mkiwa ni Swalihina basi hakika Yeye daima Ni Mwingi wa Kughufuria wenye kutubia kila mara Kwake.

 

 

 

وَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا ﴿٢٦﴾

26. Na mpe jamaa wa karibu haki yake, na masikini, na msafiri (aliyeharibikiwa), na wala usifanye ubadhirifu[3] wa ufujaji mkubwa. 

 

 

 

إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ ۖ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِرَبِّهِ كَفُورًا ﴿٢٧﴾

27. Hakika wabadhirifu wamekuwa ni ndugu wa mashaytwaan, na shaytwaan amekuwa ni mwingi wa kumkufuru Rabb wake.

 

 

 

وَإِمَّا تُعْرِضَنَّ عَنْهُمُ ابْتِغَاءَ رَحْمَةٍ مِّن رَّبِّكَ تَرْجُوهَا فَقُل لَّهُمْ قَوْلًا مَّيْسُورًا ﴿٢٨﴾

28. Na kama unajikurupusha nao na huku unatafuta Rahmah ya Rabb wako unayoitaraji, basi sema nao kauli laini.

 

 

 

وَلَا تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً إِلَىٰ عُنُقِكَ وَلَا تَبْسُطْهَا كُلَّ الْبَسْطِ فَتَقْعُدَ مَلُومًا مَّحْسُورًا ﴿٢٩﴾

29. Na wala usifanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako (ubakhili), na wala usiukunjue wote kabisa (kwa ubadhirifu) ukaja kubakia mwenye kulaumiwa, mwenye kufilisika.

 

 

 

إِنَّ رَبَّكَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا ﴿٣٠﴾

30. Hakika Rabb wako Hukunjua riziki kwa Amtakaye na Hubana (kwa Amtakaye). Hakika Yeye daima kwa Waja Wake Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na za siri, Mwenye Kuona yote.

 

 

 

 

وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُمْ ۚ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْئًا كَبِيرًا ﴿٣١﴾

31. Na wala msiue watoto wenu kwa kukhofia ufukara. Sisi Tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua imekuwa ni hatia kubwa.

 

 

 

وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٣٢﴾

32. Na wala msiikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya kabisa.

 

 

 

وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِف فِّي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنصُورًا ﴿٣٣﴾

33. Na wala msiue nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuiua) isipokuwa kwa haki. Na atakayeuliwa kwa kudhulumiwa, basi Tumemfanya mrithi wake awe na mamlaka.  Lakini asipindukie mipaka katika kuua. Hakika yeye atasaidiwa (kwa Shariy’ah).

 

 

 

وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۚ وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا ﴿٣٤﴾

34. Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan mpaka afikie umri wa kupevuka. Na timizeni ahadi, hakika ahadi itakuwa ni ya kuulizwa.

 

 

 

وَأَوْفُوا الْكَيْلَ إِذَا كِلْتُمْ وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٣٥﴾

35. Na timizeni kamilifu kipimo mnapopima, na pimeni kwa kipimo cha sawasawa. Hivyo ni kheri na bora zaidi matokeo yake.

 

 

 

وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾

36. Na wala usifuate usiyo na elimu nayo. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitaulizwa.

 

 

 

وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّكَ لَن تَخْرِقَ الْأَرْضَ وَلَن تَبْلُغَ الْجِبَالَ طُولًا ﴿٣٧﴾

37. Na wala usitembee katika ardhi kwa majivuno. Hakika wewe huwezi kupasua ardhi, na wala huwezi kufikia urefu wa milima.

 

 

 

كُلُّ ذَٰلِكَ كَانَ سَيِّئُهُ عِندَ رَبِّكَ مَكْرُوهًا ﴿٣٨﴾

38. Yote hayo, uovu wake umekuwa ni wa kukirihisha mbele ya Rabb wako.

 

 

 

ذَٰلِكَ مِمَّا أَوْحَىٰ إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ الْحِكْمَةِ ۗ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتُلْقَىٰ فِي جَهَنَّمَ مَلُومًا مَّدْحُورًا ﴿٣٩﴾

39. Hayo ni miongoni mwa hikmah ambayo Amekufunulia Wahy Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na wala usifanye pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine ukaja kutupwa katika Jahannam hali ya kuwa mwenye kulaumiwa na kufukuziliwa mbali. 

 

 

 

أَفَأَصْفَاكُمْ رَبُّكُم بِالْبَنِينَ وَاتَّخَذَ مِنَ الْمَلَائِكَةِ إِنَاثًا ۚ إِنَّكُمْ لَتَقُولُونَ قَوْلًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾

40. Je, Rabb wenu Amekukhitarieni watoto wa kiume na Yeye Amejichukulia Malaika watoto wa kike? Hakika nyinyi mnasema kauli nzito mno![4]

 

 

 

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ لِيَذَّكَّرُوا وَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا نُفُورًا ﴿٤١﴾

41. Na kwa yakini Tumesarifu namna kwa namna katika hii Qur-aan ili wakumbuke, lakini haiwazidishii ila kukimbia (haki) kwa chuki.

 

 

 

قُل لَّوْ كَانَ مَعَهُ آلِهَةٌ كَمَا يَقُولُونَ إِذًا لَّابْتَغَوْا إِلَىٰ ذِي الْعَرْشِ سَبِيلًا ﴿٤٢﴾

42. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama wangelikuwa pamoja Naye waabudiwa kama wasemavyo, basi hapo wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye ‘Arshi.[5]

 

 

 

سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَقُولُونَ عُلُوًّا كَبِيرًا ﴿٤٣﴾

43. Subhaanahu wa Ta’aalaa! (Ametakasika Allaah na Ametukuka) kutokana na wanayoyasema ya uongo na dhulma kubwa ya hali ya juu kabisa!

 

 

 

تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤٤﴾

44. Zinamsabihi mbingu saba na ardhi na waliomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinasabihi na kumhimidi Yeye, lakini hamzifahamu tasbiyh zao. Hakika Yeye Ni Mvumilivu, Mwingi wa Kughufuria.

 

 

 

وَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ جَعَلْنَا بَيْنَكَ وَبَيْنَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ حِجَابًا مَّسْتُورًا ﴿٤٥﴾

45. Na unaposoma Qur-aan Tunajaalia baina yako na baina ya wale wasioamini Aakhirah kizuizi kinachofunika.

 

 

 

وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِذَا ذَكَرْتَ رَبَّكَ فِي الْقُرْآنِ وَحْدَهُ وَلَّوْا عَلَىٰ أَدْبَارِهِمْ نُفُورًا ﴿٤٦﴾

46. Na Tumetia juu ya nyoyo zao vifuniko wasiifahamu, na katika masikio yao uziwi. Na unapomtaja Rabb wako katika Qur-aan Pekee wanageuza migongo kukimbia (haki) kwa chuki.[6]

 

 

 

نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَسْتَمِعُونَ بِهِ إِذْ يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ وَإِذْ هُمْ نَجْوَىٰ إِذْ يَقُولُ الظَّالِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا مَّسْحُورًا ﴿٤٧﴾

47. Sisi Tunajua zaidi kile wanacholenga kukisikiliza pale wanapokusikiliza kwa makini, na wakati wanaponong’ona.  (Na Tunajua pia) wanaposema madhalimu: Hamfuati isipokuwa mtu aliyefanyiwa sihri.

 

 

 

انظُرْ كَيْفَ ضَرَبُوا لَكَ الْأَمْثَالَ فَضَلُّوا فَلَا يَسْتَطِيعُونَ سَبِيلًا ﴿٤٨﴾

48. Tazama vipi walivyokupigia mifano wakapotoka, basi hawawezi kupata njia (ya kuwahidi).

 

 

 

وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا ﴿٤٩﴾

49. Na wakasema: Je, hivi sisi tukiwa mifupa, na mapande yaliyosagika sagika, je, hivi sisi hivyo tutafufuliwa katika umbo jipya?[7]

 

 

 

قُلْ كُونُوا حِجَارَةً أَوْ حَدِيدًا ﴿٥٠﴾

50. Sema: Kuweni mawe au chuma.

 

 

 

أَوْ خَلْقًا مِّمَّا يَكْبُرُ فِي صُدُورِكُمْ ۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَا ۖ قُلِ الَّذِي فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَ ۖ قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ قَرِيبًا ﴿٥١﴾

51. Au umbo katika vile vinavyohisiwa vikubwa (au vigumu) katika vifua vyenu. Basi watasema: Nani atakayeturudisha (kuwa hai?). Sema: Ni Yule Aliyekuanzisheni mara ya kwanza! Basi watakutingishia vichwa vyao na kusema: Lini hayo?! Sema: Asaa yawe karibu.

 

 

 

يَوْمَ يَدْعُوكُمْ فَتَسْتَجِيبُونَ بِحَمْدِهِ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٥٢﴾

52. Siku Atakayokuiteni, nanyi mtamuitika huku mkimhimidi, na mtaona kama vile hamkubakia (duniani) isipokuwa kidogo tu.

 

 

 

وَقُل لِّعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنزَغُ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوًّا مُّبِينًا ﴿٥٣﴾

53. Na waambie Waja Wangu waseme maneno yaliyo mazuri zaidi. Hakika shaytwaan anachochea baina yao. Hakika shaytwaan kwa binaadamu daima ni adui bayana.

 

 

 

رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِكُمْ ۖ إِن يَشَأْ يَرْحَمْكُمْ أَوْ إِن يَشَأْ يُعَذِّبْكُمْ ۚ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا ﴿٥٤﴾

54. Rabb wenu Anakujueni vizuri zaidi. Akitaka Atakurehemuni au Akitaka Atakuadhibuni. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa mlinzi wao.

 

 

 

وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِمَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ النَّبِيِّينَ عَلَىٰ بَعْضٍ ۖ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿٥٥﴾

55. Na Rabb wako Anawajua vilivyo waliomo katika mbingu na ardhi. Na kwa yakini Tumewafadhilisha baadhi ya Manabii juu ya wengineo. Na Tukampa Daawuwd Zabuwr.

 

 

 

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾

56. Sema: Iteni wale ambao mnadai (ni waabudiwa) pasi Naye, basi hawamiliki uwezo wa kukuondosheeni dhara wala kuihamisha (kwa mwengine).

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾

57. Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi, na wanataraji Rahmah Yake, na wanakhofu Adhabu Yake. Hakika Adhabu ya Rabb wako ni ya kutahadhariwa daima.

 

 

 

وَإِن مِّن قَرْيَةٍ إِلَّا نَحْنُ مُهْلِكُوهَا قَبْلَ يَوْمِ الْقِيَامَةِ أَوْ مُعَذِّبُوهَا عَذَابًا شَدِيدًا ۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا ﴿٥٨﴾

58. Na hakuna mji wowote isipokuwa Sisi Tutauangamiza kabla ya Siku ya Qiyaamah, au Tutauadhibu adhabu kali. Hayo yameandikwa katika Kitabu (Lawh Al-Mahfuwdhw)[8].

 

 

 

وَمَا مَنَعَنَا أَن نُّرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَن كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا ﴿٥٩﴾

59. Na hakuna kinachotuzuia kuleta Muujiza isipokuwa ni kuwa watu wa awali waliikadhibisha. Na Tuliwapa kina Thamuwd ngamia jike kuwa dalili dhahiri lakini wakamdhulumu. Na Hatupeleki Miujiza na maonyo isipokuwa kwa ajili ya kukhofisha.

 

 

 

وَإِذْ قُلْنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِالنَّاسِ ۚ وَمَا جَعَلْنَا الرُّؤْيَا الَّتِي أَرَيْنَاكَ إِلَّا فِتْنَةً لِّلنَّاسِ وَالشَّجَرَةَ الْمَلْعُونَةَ فِي الْقُرْآنِ ۚ وَنُخَوِّفُهُمْ فَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا طُغْيَانًا كَبِيرًا ﴿٦٠﴾

60. Na (kumbuka ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Tulipokuambia: Hakika Rabb wako Amekwishawazunguka watu. Na Hatukuijaalia ndoto ambayo Tulikuonyesha isipokuwa ni mtihani kwa watu, na mti uliolaaniwa katika Qur-aan. Na Tunawatisha, basi haiwazidishii isipokuwa upindukaji mipaka mkubwa wa kuasi.[9]

 

 

 

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ قَالَ أَأَسْجُدُ لِمَنْ خَلَقْتَ طِينًا ﴿٦١﴾

61. Na pindi Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys. Akasema: Je, nimsujudie Uliyemuumba kwa udongo?[10]

 

 

 

قَالَ أَرَأَيْتَكَ هَـٰذَا الَّذِي كَرَّمْتَ عَلَيَّ لَئِنْ أَخَّرْتَنِ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَأَحْتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٦٢﴾

62. (Ibliys) Akasema: Unamwona huyu ambaye Umemkirimu zaidi yangu! Basi Ukiniakhirisha mpaka Siku ya Qiyaamah, bila shaka nitaangamiza kabisa kizazi chake isipokuwa wachache.

 

 

 

قَالَ اذْهَبْ فَمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَاؤُكُمْ جَزَاءً مَّوْفُورًا ﴿٦٣﴾

63. (Allaah) Akasema: Nenda! Kwani atakayekufuata miongoni mwao, basi hakika Jahannam ni jazaa yenu, jazaa timilifu.

 

 

 

وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُم بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ وَعِدْهُمْ ۚ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا ﴿٦٤﴾

64. Na wachochee kilaini uwawezao miongoni mwao kwa sauti yako, na wakusanyie kikosi chako cha farasi, na askari wako waendao kwa miguu, na shirikiana nao katika mali na watoto na waahidi. Lakini shaytwaan hawapi ahadi isipokuwa ni udanganyifu.

 

 

 

إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ ۚ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ وَكِيلًا ﴿٦٥﴾

65. Hakika Waja Wangu huna mamlaka juu yao. Na Rabb wako Anatosheleza Kuwa Mtegemewa.

 

 

 

 

رَّبُّكُمُ الَّذِي يُزْجِي لَكُمُ الْفُلْكَ فِي الْبَحْرِ لِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٦٦﴾

66. Rabb wenu Ndiye Ambaye Anakuendesheeni merikebu baharini ili mtafute Fadhila Zake. Hakika Yeye Ni Mwenye Kukurehemuni.

 

 

 

وَإِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فِي الْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّا إِيَّاهُ ۖ فَلَمَّا نَجَّاكُمْ إِلَى الْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ كَفُورًا ﴿٦٧﴾

67. Na inapokuguseni dhara baharini wale mnaowaomba hupotea isipokuwa Yeye Pekee. Anapokuokoeni katika nchi kavu mnakengeuka. Na binaadamu amekuwa ni mwingi wa kukufuru, asiyeshukuru.

 

 

 

أَفَأَمِنتُمْ أَن يَخْسِفَ بِكُمْ جَانِبَ الْبَرِّ أَوْ يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ثُمَّ لَا تَجِدُوا لَكُمْ وَكِيلًا ﴿٦٨﴾

68. Je, mmeaminisha kwamba (Allaah) Hatokudidimizeni upande wowote wa nchi kavu, au Hatokuleteeni tufani ya mawe, kisha hamtopata wa kumtegemea? 

 

 

 

أَمْ أَمِنتُمْ أَن يُعِيدَكُمْ فِيهِ تَارَةً أُخْرَىٰ فَيُرْسِلَ عَلَيْكُمْ قَاصِفًا مِّنَ الرِّيحِ فَيُغْرِقَكُم بِمَا كَفَرْتُمْ ۙ ثُمَّ لَا تَجِدُوا لَكُمْ عَلَيْنَا بِهِ تَبِيعًا ﴿٦٩﴾

69. Au je, mmeaminisha kwamba (Allaah) Hatokurudisheni huko (baharini) mara nyingine, kisha Akakutumieni kimbunga cha upepo Akakugharikisheni kwa sababu ya kufru yenu kisha hamtopata mteteaji wa kukunusuruni Nasi? 

 

 

 

وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا ﴿٧٠﴾

70. Na kwa yakini Tumewakirimu wana wa Aadam, na Tukawabeba katika nchi kavu na baharini, na Tukawaruzuku katika vizuri na Tukawafadhilisha juu ya wengi miongoni mwa Tuliowaumba kwa ufadhilisho mkubwa.

 

 

 

يَوْمَ نَدْعُو كُلَّ أُنَاسٍ بِإِمَامِهِمْ ۖ فَمَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَأُولَـٰئِكَ يَقْرَءُونَ كِتَابَهُمْ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٧١﴾

71. Siku Tutakayoita watu wote pamoja na rekodi zao za matendo (au Nabii wao). Basi atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, hao watasoma kitabu chao na wala hawatodhulumiwa kadiri ya uzi katika kokwa ya tende.[11] 

 

 

 

 

 

وَمَن كَانَ فِي هَـٰذِهِ أَعْمَىٰ فَهُوَ فِي الْآخِرَةِ أَعْمَىٰ وَأَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٧٢﴾

72. Na atakayekuwa kipofu katika hii (dunia) basi yeye Aakhirah atakuwa kipofu na atapotea zaidi njia. 

 

 

 

وَإِن كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ ۖ وَإِذًا لَّاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا ﴿٧٣﴾

73. Na hakika walikaribia kukukengeusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale Tuliyokufunulia Wahy ili upate kututungia mengineyo. Basi hapo ndipo wangelikufanya rafiki mwandani.

 

 

 

وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا ﴿٧٤﴾

74. Na lau kama Hatukukuthibitisha, kwa yakini ungelikaribia kuelemea kwao kidogo.

 

 

 

إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا ﴿٧٥﴾

75.  Hapo basi bila shaka Tungelikuonjesha (adhabu) maradufu ya uhai na (adhabu) maradufu ya mauti kisha usingelipata wa kukunusuru Nasi.

 

 

 

وَإِن كَادُوا لَيَسْتَفِزُّونَكَ مِنَ الْأَرْضِ لِيُخْرِجُوكَ مِنْهَا ۖ وَإِذًا لَّا يَلْبَثُونَ خِلَافَكَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٧٦﴾

76. Na hakika walikaribia wakusumbue mno katika nchi ili wakutoe humo. Na hapo wao wasingelibakia baada yako isipokuwa kidogo tu.

 

 

 

سُنَّةَ مَن قَدْ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِن رُّسُلِنَا ۖ وَلَا تَجِدُ لِسُنَّتِنَا تَحْوِيلًا ﴿٧٧﴾

77. (Hiyo ndiyo) Desturi ya Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Rusuli Wetu. Na wala hutopata mabadiliko katika desturi Zetu.[12]

 

 

 

 

أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا ﴿٧٨﴾

78. Simamisha Swalaah jua linapopinduka hadi kiza cha usiku na Qur-aan ya (Swalaah ya) Alfajiri. Hakika Qur-aan ya Alfajiri ni yenye kushuhudiwa.

 

 

 

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾

79. Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kwa kuisoma (Qur-aan) ikiwa ni ziada kwako. Asaa Rabb wako Akakuinua cheo cha kuhimidiwa (kusifika).[13]

 

 

 

 

وَقُل رَّبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا ﴿٨٠﴾

80. Na sema: Ee Rabb wangu! Niingize mwingizo wa kheri na Nitoe pa kutokea pa kheri na Nijaalie kutoka Kwako (hoja au) mamlaka yenye kunusuru.

 

 

 

وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۚ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا ﴿٨١﴾

81. Na sema: Haki imekuja, na ubatili umetoweka. Hakika ubatili ni wenye kutoweka daima.

 

 

 

وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا ﴿٨٢﴾

82. Na Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na Rahmah kwa Waumini, na wala haiwazidishii madhalimu isipokuwa khasara.

 

 

 

وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ ۖ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ كَانَ يَئُوسًا ﴿٨٣﴾

83. Na Tunapomneemesha bin Aadam, hukengeuka na kujitenga mbali, lakini inapomgusa shari, huwa mwenye kukata tamaa.

 

 

 

قُلْ كُلٌّ يَعْمَلُ عَلَىٰ شَاكِلَتِهِ فَرَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَنْ هُوَ أَهْدَىٰ سَبِيلًا ﴿٨٤﴾

84. Sema: Kila mmoja anatenda kwa namna yake. Basi Rabb wenu Anamjua zaidi yule aliyeongoka zaidi katika njia (ya haki).

 

 

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾

85. Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: Roho ni katika Jambo la Rabb wangu. Na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu.

 

 

 

وَلَئِن شِئْنَا لَنَذْهَبَنَّ بِالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ بِهِ عَلَيْنَا وَكِيلًا ﴿٨٦﴾

86. Na kama Tungelitaka, bila shaka Tungeliondosha yale Tuliyokufunulia Wahy, kisha usingelipata kwa haya, mtegemewa wa kukunusuru Nasi.

 

 

 

إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّ فَضْلَهُ كَانَ عَلَيْكَ كَبِيرًا ﴿٨٧﴾

87. Isipokuwa Rahmah kutoka kwa Rabb wako. Hakika Fadhila Zake juu yako daima ni kubwa.

 

 

 

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾

88. Sema: Ikiwa watajumuika wana Aadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan, hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao.[14]

 

 

 

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ فَأَبَىٰ أَكْثَرُ النَّاسِ إِلَّا كُفُورًا ﴿٨٩﴾

89. Na kwa yakini Tumesarifu namna kwa namna hii Qur-aan kwa watu, kwa kila mfano, lakini watu wengi wamekataa kabisa (haki; hawakukubali) isipokuwa kukufuru tu.

 

 

 

وَقَالُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفْجُرَ لَنَا مِنَ الْأَرْضِ يَنبُوعًا ﴿٩٠﴾

90. Na wakasema: Hatutakuamini (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mpaka utububujie kutoka ardhini chemchemu.

 

 

 

أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ الْأَنْهَارَ خِلَالَهَا تَفْجِيرًا ﴿٩١﴾

91. Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, kisha utububujie mito kati yake mbubujiko mkubwa.

 

 

 

أَوْ تُسْقِطَ السَّمَاءَ كَمَا زَعَمْتَ عَلَيْنَا كِسَفًا أَوْ تَأْتِيَ بِاللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ قَبِيلًا ﴿٩٢﴾

92. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai, au umlete Allaah na Malaika uso kwa uso.

 

 

 

أَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِّن زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَىٰ فِي السَّمَاءِ وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَّقْرَؤُهُ ۗ قُلْ سُبْحَانَ رَبِّي هَلْ كُنتُ إِلَّا بَشَرًا رَّسُولًا ﴿٩٣﴾

93. Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upande mbinguni. Na wala hatutoamini kamwe kupanda kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome.  Sema: Utakasifu ni wa Rabb wangu! Kwani mimi nimekuwa nani isipokuwa ni binaadamu (na) Rasuli!

 

 

 

وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ إِلَّا أَن قَالُوا أَبَعَثَ اللَّـهُ بَشَرًا رَّسُولًا ﴿٩٤﴾

94. Na hakuna kilichowazuia watu wasiamini ulipowajia mwongozo isipokuwa husema: Je, Allaah Ametuma binaadamu kuwa ni Rasuli?

 

 

 

قُل لَّوْ كَانَ فِي الْأَرْضِ مَلَائِكَةٌ يَمْشُونَ مُطْمَئِنِّينَ لَنَزَّلْنَا عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ مَلَكًا رَّسُولًا ﴿٩٥﴾

95. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama ingelikuwa katika ardhi kuna Malaika wanatembea kwa utulivu na amani; basi bila shaka Tungeliwateremshia kutoka mbinguni Malaika kuwa ni Rasuli.

 

 

 

قُلْ كَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا ﴿٩٦﴾

96. Sema: Anatosheleza Allaah kuwa Shahidi baina yangu na baina yenu. Hakika Yeye daima Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na za siri za Waja Wake, Mwenye Kuona yote.

 

 

 

وَمَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِهِ ۖ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَّأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا ﴿٩٧﴾

97. Na ambaye Allaah Amemhidi, basi huyo ndiye aliyehidika. Na Anayempotoa, basi hutowapatia walinzi pasi Naye. Na Tutawakusanya Siku ya Qiyaamah juu ya nyuso zao (wakiwa) vipofu, mabubu na viziwi, makazi yao ni (moto wa) Jahannam, kila ukififia Tutawazidishia moto uliowashwa vikali mno.

 

 

 

ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُم بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا ﴿٩٨﴾

98. Hiyo ndiyo jazaa yao kwa kuwa wao walizikanusha Aayaat na Ishara Zetu na wakasema: Je, hivi sisi tukiwa mifupa na mapande yaliyosagika sagika, hivi kweli sisi tutafufuliwa katika umbo jipya?

 

 

 

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَّا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى الظَّالِمُونَ إِلَّا كُفُورًا ﴿٩٩﴾

99. Je, hawajaona kwamba Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi Ni Mweza wa Kuumba mfano wao?  Na Amewawekea muda maalumu usio na shaka? Lakini madhalimu wamekataa kabisa hawana isipokuwa kukufuru tu.

 

 

 

قُل لَّوْ أَنتُمْ تَمْلِكُونَ خَزَائِنَ رَحْمَةِ رَبِّي إِذًا لَّأَمْسَكْتُمْ خَشْيَةَ الْإِنفَاقِ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ قَتُورًا ﴿١٠٠﴾

100. Sema: Ingekuwa nyinyi mnamiliki hazina za Rahmah ya Rabb wangu bila shaka hapo mngelizuia kuzitumia kwa ajili ya kukhofu (zisimalizike). Na binaadamu amekuwa ni mchoyo kupindukia.

 

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ تِسْعَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ فَاسْأَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ إِذْ جَاءَهُمْ فَقَالَ لَهُ فِرْعَوْنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا مُوسَىٰ مَسْحُورًا ﴿١٠١﴾

101. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Miujiza tisa bayana. Basi waulize wana wa Israaiyl alipowajia, na Fir’awn akamwambia: Hakika mimi nakuona ewe Muwsaa kuwa umerogwa.

 

 

 

قَالَ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنزَلَ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ بَصَائِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا فِرْعَوْنُ مَثْبُورًا ﴿١٠٢﴾

102. (Muwsaa) Akasema: Kwa yakini umekwishajua kwamba hakuna Aliyeteremsha haya isipokuwa Rabb wa mbingu na ardhi kuwa ni dalili za kuonekana dhahiri, na hakika mimi bila shaka nakuona ewe Fir’awn kuwa umekwisha angamia.

 

 

 

فَأَرَادَ أَن يَسْتَفِزَّهُم مِّنَ الْأَرْضِ فَأَغْرَقْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ جَمِيعًا ﴿١٠٣﴾

103. Basi akataka awasumbue na kuwafukuza katika nchi, Tukamgharikisha yeye na waliokuwa pamoja naye wote.

 

 

 

وَقُلْنَا مِن بَعْدِهِ لِبَنِي إِسْرَائِيلَ اسْكُنُوا الْأَرْضَ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا ﴿١٠٤﴾

104. Na Tukawaambia baada yake wana wa Israaiyl: Kaeni katika ardhi, na itakapokuja ahadi ya Aakhirah Tutakuleteni nyote pamoja kwa makundi mchanganyiko.

 

 

 

وَبِالْحَقِّ أَنزَلْنَاهُ وَبِالْحَقِّ نَزَلَ ۗ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿١٠٥﴾

105. Na kwa haki Tumeiteremsha (Qur-aan), na kwa haki imeteremka. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni mbashiriaji na mwonyaji tu.

 

 

 

وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ تَنزِيلًا ﴿١٠٦﴾

106. Na Qur-aan Tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na Tumeiteremsha kidogo kidogo.

 

 

 

قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا ﴿١٠٧﴾

107. Sema: Iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake wanaposomewa (Qur-aan) wanaporomoka kifudifudi wanasujudu.

 

 

 

وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا ﴿١٠٨﴾

108. Na wanasema: Utakasifu ni wa Rabb wetu, hakika Ahadi ya Rabb wetu lazima itimizwe.

 

 

 

وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩﴿١٠٩﴾

109. Na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu.

 

 

 

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١١٠﴾

110. Sema: Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. Na wala usisome kwa sauti ya juu katika Swalaah yako wala kwa sauti ya chini sana, bali shika njia ya wastani baina yake.

 

 

 

 

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖ وَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا ﴿١١١﴾

111. Na sema: AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Ambaye Hakujifanyia mwana na wala Hakuwa na mshirika katika ufalme, na wala Hakuwa dhalili hata Awe (Anahitaji) mlinzi msaidizi, na mtukuze matukuzo makubwa kabisa.[15]  

 

 

 

 

 

 

 

 

Share