056 - Al-Waaqi'ah

 

 

 

   الْوَاقِعَة

Al-Waaqi’ah: 056

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ ﴿١﴾

1. Litakapotokea Tukio!

 

 

لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ ﴿٢﴾

2. Hakuna cha kukadhibisha kutokea kwake.

 

 

خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ ﴿٣﴾

3. Literemshalo hadhi na linyanyualo hadhi.

 

 

إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا ﴿٤﴾

4. Itakapotikiswa ardhi mtikiso mkubwa.

 

 

وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا ﴿٥﴾

5. Na milima itakapopondwa pondwa.

 

 

فَكَانَتْ هَبَاءً مُّنبَثًّا ﴿٦﴾

6. Ikawa chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zikitawanyika.  

 

 

وَكُنتُمْ أَزْوَاجًا ثَلَاثَةً ﴿٧﴾

7. Na mtakuwa namna tatu.

 

 

فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿٨﴾

8. Basi wapo watu wa kuliani; je, ni nani watu wa kuliani?

 

 

وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿٩﴾

9. Na watu wa kushotoni; je, ni nani watu wa kushotoni?

 

 

وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ ﴿١٠﴾

10. Na waliotangulia mbele, watatangulia mbele.

 

 

أُولَـٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ ﴿١١﴾

11. Hao ndio watakaokurubishwa.

 

 

فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿١٢﴾

12. Katika Jannaat za taanisi.

 

 

ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾

13. Kundi kubwa katika wa awali.

 

وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ ﴿١٤﴾

14. Na wachache katika wa mwishoni.

 

عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ ﴿١٥﴾

15. (Watakuwa) juu ya makochi ya fakhari yaliyotariziwa na kutonewa johari za thamani kwa ustadi wa hali ya juu.

 

 

مُّتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ ﴿١٦﴾

16. Wakiegemea juu yake wakielekeana.

 

 

يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ ﴿١٧﴾

17. Watazungukiwa (kuhudumiwa) na vijana wenye kudumu (katika hali yao milele).

 

 

بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ﴿١٨﴾

18. Kwa bilauri na mabirika na vikombe vya mvinyo kutoka chemchemu inayobubujika.

 

 

لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ ﴿١٩﴾

19. Hawatoumizwa vichwa kwavyo na wala hawatoleweshwa.

 

 

وَفَاكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ ﴿٢٠﴾

20. Na matunda watakayopendelea.

 

 

وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٢١﴾

21. Na nyama za ndege katika watakazozitamani.

 

 

وَحُورٌ عِينٌ ﴿٢٢﴾

22. Na Hurulaini: Wanawake weupe wazuri wa Jannah wenye macho makubwa ya kupendeza.

 

 

كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ ﴿٢٣﴾

23. Kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa.

 

 

جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٤﴾

24. Jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda.

 

 

لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا ﴿٢٥﴾

25. Hawatosikia humo upuuzi na wala yanayosababisha dhambi.

 

 

إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا ﴿٢٦﴾

26. Isipokuwa itasemwa: Salama, salama!  

 

 

وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ ﴿٢٧﴾

27. Na watu wa kuliani, je, ni nani watu wa kuliani?

 

 

فِي سِدْرٍ مَّخْضُودٍ ﴿٢٨﴾

28. (Watakuwa) kwenye mikunazi iliyokatwa miba.

 

 

وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ ﴿٢٩﴾

29. Na migomba ya ndizi iliyopangwa matabaka.

 

 

وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ ﴿٣٠﴾

30. Na kivuli kilichotandazwa.

 

 

وَمَاءٍ مَّسْكُوبٍ ﴿٣١﴾

31. Na maji yenye kumiminwa.

 

 

وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ ﴿٣٢﴾

32. Na matunda mengi.

 

 

لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ ﴿٣٣﴾

33. Hayana kikomo na wala hayakatazwi.

 

 

وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ ﴿٣٤﴾

34. Na matandiko ya kupumzikia yaliyoinuliwa.

 

 

إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً ﴿٣٥﴾

35. Hakika Sisi Tutawaumba (hurulaini) upya tofauti na mwanzo.

 

 

فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا ﴿٣٦﴾

36. Tuwafanye mabikra.

 

 

عُرُبًا أَتْرَابًا ﴿٣٧﴾

37. Wenye mahaba, ashiki na bashasha kwa waume zao, hirimu moja.

 

 

لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٣٨﴾

38. Kwa ajili ya watu wa kuliani.

 

 

ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿٣٩﴾

39. Kundi kubwa katika wa awali.

 

 

وَثُلَّةٌ مِّنَ الْآخِرِينَ ﴿٤٠﴾

40. Na kundi kubwa katika wa mwishoni.

 

 

وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ ﴿٤١﴾

41. Na watu wa kushotoni, je, ni nani watu wa kushotoni?

 

 

فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ ﴿٤٢﴾

42. (Watakuwa) kwenye moto ubabuao na maji yachemkayo.

 

 

وَظِلٍّ مِّن يَحْمُومٍ ﴿٤٣﴾

43. Na kivuli cha moshi mweusi mnene wa joto kali mno.

 

 

لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ ﴿٤٤﴾

44. Si cha baridi na wala si cha kunufaisha.

 

 

إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ ﴿٤٥﴾

45. Hakika wao walikuwa kabla ya hayo wanaostareheshwa kwa anasa za dunia.

 

 

 

وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنثِ الْعَظِيمِ ﴿٤٦﴾

46. Na walikuwa wakishikilia kufanya dhambi kubwa mno.

 

 

وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿٤٧﴾

47. Na walikuwa wakisema: Je, hivi tutakapokufa na tukawa udongo na mifupa, je hivi sisi hakika tutafufuliwa?

 

 

أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ ﴿٤٨﴾

48. Au, je na baba zetu wa awali pia?

 

 

قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ ﴿٤٩﴾

49. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika wa awali na wa mwishoni.

 

 

لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿٥٠﴾

50. Bila shaka watajumuishwa katika wakati na mahali pa siku maalumu.

 

 

ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ ﴿٥١﴾

51. Kisha hakika nyinyi enyi wapotovu mnaokadhibisha.

 

 

لَآكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ ﴿٥٢﴾

52. Bila shaka mtakula katika mti wa zaqquwm.

 

 

فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٥٣﴾

53. Na kwa huo mtajaza matumbo.

 

 

فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ ﴿٥٤﴾

54. Na mtakunywa juu yake maji ya moto yachemkayo mno.

 

 

فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ ﴿٥٥﴾

55. Tena mtakunywa kama wanywavyo ngamia wenye kiu mno!

 

 

هَـٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ ﴿٥٦﴾

56. Haya ndio mapokezi yao Siku ya Malipo!

 

 

نَحْنُ خَلَقْنَاكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ ﴿٥٧﴾

57. Sisi Tumekuumbeni, basi kwa nini hamsadiki?

 

 

أَفَرَأَيْتُم مَّا تُمْنُونَ ﴿٥٨﴾

58. Je, basi mnaona manii mnayoimwagia kwa nguvu?

 

 

 

أَأَنتُمْ تَخْلُقُونَهُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ ﴿٥٩﴾

59. Je, nyinyi ndio mnayoiumba au Sisi ndio Waumbaji?

 

 

نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ ﴿٦٠﴾

60. Sisi Tumekadiria baina yenu mauti, Nasi Sio Wenye Kushindwa.

 

 

عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦١﴾

61. Kwamba Tuwabadilishe wengine mifano yenu, na Tukuumbeni katika umbo msilolijua.

 

 

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾

62. Na bila shaka mmejua umbo la awali, basi kwa nini hamkumbuki?

 

 

أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ ﴿٦٣﴾

63. Je, mnaona mbegu mnazozipanda? 

 

 

أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ ﴿٦٤﴾

64. Je, ni nyinyi ndio mnaziotesha, au Sisi Ndio Wenye Kuotesha mimea?

 

 

 

لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ ﴿٦٥﴾

65. Lau Tungelitaka, Tungeliifanya mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka, mkabaki mnashangaa na kusikitika.

 

 

إِنَّا لَمُغْرَمُونَ ﴿٦٦﴾

66. (Mkisema): Hakika sisi tumegharimika.

 

 

بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ ﴿٦٧﴾

67. Bali sisi tumenyimwa.

 

 

أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ ﴿٦٨﴾

68. Je, mnaona maji ambayo mnakunywa?

 

 

أَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ ﴿٦٩﴾

69. Je, ni nyinyi ndio mliyoyateremsha kutoka katika mawingu ya mvua au Sisi Ndio Wateremshaji?

 

 

لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ ﴿٧٠﴾

70. Lau Tungelitaka, Tungeliyafanya ya chumvi kali chungu, basi kwa nini hamshukuru?!

 

 

أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ ﴿٧١﴾

71. Je, mnaona moto ambao mnauwasha?

 

 

أَأَنتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنشِئُونَ ﴿٧٢﴾

72. Je, ni nyinyi ndio mliouanzisha mti wake, au Sisi Ndio Waanzilishaji?

 

 

نَحْنُ جَعَلْنَاهَا تَذْكِرَةً وَمَتَاعًا لِّلْمُقْوِينَ ﴿٧٣﴾

73. Sisi Tumeufanya kuwa ni ukumbusho na manufaa kwa wasafiri katika jangwa na wahitaji.

 

 

فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾

74. Basi sabbih kwa Jina la Rabb wako Mwenye U’adhwama.

 

 

فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ ﴿٧٥﴾

75. Basi Naapa kwa maanguko ya nyota.

 

 

وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ ﴿٧٦﴾

76. Na hakika hicho ni kiapo adhimu lau mngelijua.

 

 

إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ﴿٧٧﴾

77. Hakika hii bila shaka ni Qur-aan Tukufu.

 

 

فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ ﴿٧٨﴾

78. Katika Kitabu kilichohifadhiwa.

 

 

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ ﴿٧٩﴾

79. Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa.

 

 

تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨٠﴾

80. Ni uteremsho kutoka kwa Rabb wa walimwengu.

 

 

أَفَبِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ ﴿٨١﴾

81. Je, basi kwa (unafiki na kujipendekeza) maneno haya nyinyi mnayakanusha na kuyabeza?

 

 

وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na mnafanya kuruzukiwa kwenu kuwa ndio mnakadhibisha?!

 

 

 

فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ ﴿٨٣﴾

83. Basi mbona roho ifikapo kooni.

 

 

وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ ﴿٨٤﴾

84. Nanyi wakati huo mnatazama.

 

 

وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ ﴿٨٥﴾

85. Nasi Tuko karibu naye zaidi kuliko nyinyi, lakini hamuoni.

 

 

فَلَوْلَا إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ ﴿٨٦﴾

86. Basi je, -mnaweza- ikiwa mnadai kwamba hamtohisabiwa wala kulipwa (na kwamba hamko chini ya Mamlaka Yetu).

 

 

تَرْجِعُونَهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٨٧﴾

87. Kuirudisha roho (mwilini mwake), mkiwa ni wakweli?

 

 

فَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٨٨﴾

88. Basi akiwa miongoni mwa waliokurubishwa.

 

 

فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ ﴿٨٩﴾

89. Basi mapumziko ya raha na manukato na Jannah ya neema.

 

 

وَأَمَّا إِن كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٩٠﴾

90. Na kama akiwa miongoni mwa watu wa kuliani.

 

 

فَسَلَامٌ لَّكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٩١﴾

91. Basi (ataambiwa): Salaam juu yako uliye katika watu wa kuliani.

 

 

وَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُكَذِّبِينَ الضَّالِّينَ ﴿٩٢﴾

92. Na kama akiwa miongoni mwa wakadhibishaji waliopotoka.

 

 

فَنُزُلٌ مِّنْ حَمِيمٍ ﴿٩٣﴾

93. Basi mapokezi yake ni maji ya moto yachemkayo.

 

 

وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ ﴿٩٤﴾

94. Na kuunguzwa na moto uwakao vikali mno.

 

 

إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ حَقُّ الْيَقِينِ ﴿٩٥﴾

95. Hakika hii bila shaka ni haki yenye yakini.

 

 

فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ ﴿٩٦﴾

96. Basi sabbih kwa Jina la Rabb wako Mwenye U’adhwama.  

 

 

 

Share