074 - Al-Muddaththir

 

 

 

   الْمُدَّثِّر

Al-Muddaththir: 074

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika!

 

 

قُمْ فَأَنذِرْ﴿٢﴾

2. Simama uonye.

 

 

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ﴿٣﴾

3. Na Rabb wako mtukuze. 

 

 

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ﴿٤﴾

4. Na nguo zako toharisha.

 

 

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ﴿٥﴾

5. Na masanamu na machafu endelea kuepukana nayo.

 

 

وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ﴿٦﴾

6. Na wala usifanye fadhila kwa ajili ya kutaraji kukithirishiwa.

 

 

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ﴿٧﴾

7. Na kwa ajili ya Rabb wako subiri.

 

 

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ﴿٨﴾

8. Litakapopulizwa baragumu kwa sauti kali.

 

 

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ﴿٩﴾

9. Basi hiyo itakuwa ni Siku ngumu mno.

 

 

عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ﴿١٠﴾

10. Kwa makafiri si nyepesi.

 

 

ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا﴿١١﴾

11. Niache Mimi na yule Niliyemuumba Pekee.

 

 

وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا﴿١٢﴾

12. Na Nikamjaalia mali tele.

 

 

وَبَنِينَ شُهُودًا﴿١٣﴾

13. Na watoto walio naye nyakati zote.

 

 

وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا﴿١٤﴾

14. Na Nikamkunjulia njia zote za maisha mazuri.

 

 

ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ﴿١٥﴾

15. Kisha anatumaini Nimuongezee.

 

 

كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا﴿١٦﴾

16. Laa, hasha!  Hakika yeye amekuwa anidi na mpinzani wa Aayaat Zetu.

 

 

سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا﴿١٧﴾

17. Nitamshurutisha adhabu ngumu asiyoiweza.

 

 

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ﴿١٨﴾

18. Hakika yeye alitafakari na akakadiria.   

 

 

فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ﴿١٩﴾

19. Basi alaaniwe na aangamie mbali. Namna gani kakadiria?!  

 

 

ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ﴿٢٠﴾

20. Kisha alaaniwe na aangamie mbali. Namna gani kakadiria?!

 

 

ثُمَّ نَظَرَ﴿٢١﴾

21. Kisha akatazama.

 

 

ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ﴿٢٢﴾

22. Kisha akakunja kipaji na akafinya uso kwa ghadhabu.

 

 

ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ﴿٢٣﴾

23. Kisha akageuka nyuma na akatakabari.

 

 

فَقَالَ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ﴿٢٤﴾

24. Akasema: Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni sihiri inayonukuliwa. 

 

 

إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ﴿٢٥﴾

25. Hii si chochote isipokuwa ni maneno ya binaadamu tu.

 

 

 

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ﴿٢٦﴾

26. Nitamuingiza Saqar aungue.

 

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ﴿٢٧﴾

27. Na kipi kitakachokujulisha ni nini hiyo Saqar?

 

 

لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ﴿٢٨﴾

28. (Ni moto ambao) haubakishi wala hauachi (kitu kisiunguzwe).

 

 

لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ﴿٢٩﴾

29. Wenye kubabua vibaya ngozi.

 

 

عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ﴿٣٠﴾

30. Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa.

 

 

وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ﴿٣١﴾

31. Na Hatukuweka walinzi wa moto isipokuwa ni Malaika. Na Hatukufanya idadi yao isipokuwa iwe ni jaribio kwa wale waliokufuru, ili wayakinishe wale waliopewa Kitabu, na iwazidishie iymaan wale walioamini, na wala wasitie shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini. Na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao (ya unafiki, shaka) na makafiri waseme: Allaah Amekusudia nini kwa mfano huu? Hivyo ndivyo Allaah Anavyompotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye. Na hakuna ajuaye majeshi ya Rabb wako isipokuwa Yeye Pekee. Na haya si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa binaadamu.

 

 

كَلَّا وَالْقَمَرِ﴿٣٢﴾

32. Laa, hasha! Naapa kwa mwezi.

 

 

وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ﴿٣٣﴾

33. Na Naapa kwa usiku unapoondoka.

 

 

وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ﴿٣٤﴾

34. Na Naapa kwa asubuhi inapoangaza.

 

 

إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ﴿٣٥﴾

35. Hakika huo (moto) bila shaka ni mojawapo ya majanga makubwa kabisa.

 

 

نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ﴿٣٦﴾

36. Ni onyo kwa binaadamu.

 

 

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ﴿٣٧﴾

37. Kwa atakaye miongoni mwenu atakadamu mbele au ataakhari nyuma.

 

 

 

كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ﴿٣٨﴾

38. Kila nafsi iko katika rehani kwa yale iliyoyachuma.

 

 

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ﴿٣٩﴾

39. Isipokuwa watu wa kuliani.

 

 

فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ﴿٤٠﴾

40. Katika Jannaat wanaulizana.

 

 

عَنِ الْمُجْرِمِينَ﴿٤١﴾

41. Kuhusu wahalifu.

 

 

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ﴿٤٢﴾

42. (Watawauliza): Nini kilichokuingizeni katika Saqar?

 

 

 

قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ﴿٤٣﴾

43. Watasema: Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.

 

 

وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ﴿٤٤﴾

44. Na wala hatukuwa tunalisha masikini.

 

 

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ﴿٤٥﴾

45. Na tulikuwa tunatumbukia kwenye upuuzi pamoja na wanaotumbukia upuuzini.

 

 

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ﴿٤٦﴾

46. Na tulikuwa tunaikadhibisha Siku ya malipo.

 

 

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ﴿٤٧﴾

47. Mpaka ikatufikia yakini (mauti).

 

 

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ﴿٤٨﴾

48. Basi hautowafaa uombezi wowote wa waombezi.

 

 

 

فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ﴿٤٩﴾

49. Basi wana nini hata wanaugeukilia mbali ukumbusho huu!

 

 

 

كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ﴿٥٠﴾

50. Kama kwamba ni punda milia wenye kutimuliwa.

 

 

فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ﴿٥١﴾

51. Wamekimbia mbio kutokana na wawindaji (au simba).

 

 

 

بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً﴿٥٢﴾

52. Bali anataka kila mtu miongoni mwao wao apewe sahifa zilizofunuliwa.

 

 

 

كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ﴿٥٣﴾

53. Laa, hasha! Bali hawaiogopi Aakhirah.

 

 

كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ﴿٥٤﴾

54. Laa, hasha! Hakika hii (Qur-aan) ni mawaidha. 

 

 

 

فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ﴿٥٥﴾

55. Basi anayetaka atawaidhika.

 

 

 

وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ﴿٥٦﴾

56. Na hawatowaidhika isipokuwa Akitaka Allaah. Yeye Ndiye Mstahiki wa Kuogopwa, na Mstahiki wa Kughufuria (madhambi).

 

 

 

 

Share