074-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muddath-thir Aayah 1-7: يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

 

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

074-Al-Muddath-thir Aayah 1-7

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika!

قُمْ فَأَنذِرْ﴿٢﴾

2. Simama na uonye 

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ﴿٣﴾

3. Na Rabb wako mtukuze. 

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ﴿٤﴾

4. Na nguo zako toharisha.

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ﴿٥﴾

5. Na najisi (masanamu( epukana nayo.

وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ﴿٦﴾

6. Na wala usifanye fadhila kwa ajili ya kutaraji kukithirishiwa.

 

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ﴿٧﴾

7. Na kwa ajili ya Rabb wako subiri.

 

حَدَّثَنَا يَحْيَى، حَدَّثَنَا وَكِيعٌ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ الْمُبَارَكِ،  عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ، سَأَلْتُ أَبَا سَلَمَةَ بْنَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَنْ أَوَّلِ، مَا نَزَلَ مِنَ الْقُرْآنِ‏.‏ قَالَ: ((‏يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ))  ‏قُلْتُ يَقُولُونَ ‏((‏اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ‏))‏ فَقَالَ أَبُو سَلَمَةَ: سَأَلْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ رضى الله عنهما عَنْ ذَلِكَ وَقُلْتُ لَهُ مِثْلَ الَّذِي قُلْتَ فَقَالَ جَابِرٌ: لاَ أُحَدِّثُكَ إِلاَّ مَا حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏((جَاوَرْتُ بِحِرَاءٍ، فَلَمَّا قَضَيْتُ جِوَارِي هَبَطْتُ فَنُودِيتُ فَنَظَرْتُ عَنْ يَمِينِي فَلَمْ أَرَ شَيْئًا، وَنَظَرْتُ عَنْ شِمَالِي فَلَمْ أَرَ شَيْئًا، وَنَظَرْتُ أَمَامِي فَلَمْ أَرَ شَيْئًا، وَنَظَرْتُ خَلْفِي فَلَمْ أَرَ شَيْئًا، فَرَفَعْتُ رَأْسِي فَرَأَيْتُ شَيْئًا، فَأَتَيْتُ خَدِيجَةَ فَقُلْتُ دَثِّرُونِي وَصُبُّوا عَلَىَّ مَاءً بَارِدًا)) قَالَ: ((فَدَثَّرُونِي وَصَبُّوا عَلَىَّ مَاءً بَارِدًا)) قَالَ:   فَنَزَلَتْ ((‏‏يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ * قُمْ فَأَنْذِرْ * وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ))

 

Yahyaa amenihadithia, ametuhadithia Waki’y bin ‘Aliy bin Al-Mubaarak kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr nimemuuliza Abaa Salamah bin Abdir-Rahmaah kutoka katika ya mwanzo iliyoteremka katika Qur-aan, amesema:

 

 يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika!

 

Nikasema: wanasema

 اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾

1. Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba.

 

Akasema Abuu Salamah: Nilimuuliza Jaabir kutoka kwa Abdullaah (رضي لله عنهما)  kuhusu hilo, na nikamwambia yale niliyosema, Jaabir akasema: Sikuambii isipokuwa lile ambalo ametuhadithia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba: “Nilifika (pango la) Al-Hiraa, nilipomaliza haja yangu nikaondoka. Mara nikasikia naitwa, nikageuka upande wangu wa kuume sikuona kitu, nikageuka kushoto sikuona kitu, kisha nikageuka nyuma yangu sikuona kitu, nikanyanyua kichwa changu nikaona kitu, nikaenda kwa Khadiyjah nikamwambia: Nigubike na nimwagie maji baridi!” Akasema: “Wakanigubika kisha wakanimwagia maji baridi.” Akasema ikateremka:

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika!

 

قُمْ فَأَنذِرْ﴿٢﴾

2. Simama na uonye 

 

[Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]

 

Al-Hafidhw Ibn Kathiyr amesema katika Tafsiyr (4/440) kwa maana yake: Jaabir bin Abdilaah aliikhalifu jamhuri kwa kauli yake: Kuwa ya mwanzo kushuka ilikuwa ni Suwrah Al-Muddath-thir. Na wengine walisema ya kwanza ilikuwa ni Suwrah Iqraa (Al-‘Alaq). Kisha akataja Hadiyth  katika Swahiyh mbili akasema:

 

Imepokewa na Muslim kwa njia ya ‘Uqayl kutoka kwa Ibn Shihaab kutoka kwa Abu Salamah amesema: Jaabir amenijulisha kuwa amesikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akielezea kile kipindi cha kushuka Wahyi akasema katika Hadiyth  yake: “Pindi nilipokuwa nikitembea niliposikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu upande wa mbinguni, nikamuona yule Malaika aliyenijia katika pango la Hiraa akiwa amekaa katika kitu kati ya mbingu na ardhi, nikamuelekea naye akashuka ardhini, nikaenda kwa mke wangu, nikamwambia, “Zamiluwniy! Zamiluwniy!” yaani “Nifunikeni! Nifunikeni!” hapo Allaah Akateremsha:

 يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika!

قُمْ فَأَنذِرْ﴿٢﴾

2. Simama na uonye 

 

Abuu Salamah amesema: Na rijz ni masanamu. Kisha baada ya hapo Wahyi ukaendelea kushuka na kufuatana. Hili ni tamko la Al-Bukhaariy na maelezo haya yamehifadhiwa nayo ndio yanayotarajiwa kuwa Wahyi umeteremka kabla ya kauli hii: “Mara nikamuona Malaika aliyekuwa pale pango la Hiraa” naye si mwingine bali ni Jibriyl alipomjia kwa kumteremshia: (Suwrah Al-‘Alaq : 96)

 

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾

1. Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba.

 

خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾

2. Amemuumba mwana Aadam kutokana na pande la damu linaloning’inia.

 

اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾

3. Soma na Rabb wako ni Mkarimu kushinda wote.

 

الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾

4. Ambaye Aliyefunza kwa kalamu.

 

عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾

5. Amemfunza mwana Aadam ambayo asiyoyajua.

 

Kisha baada ya hapo ikapita muda kisha Malaika akateremka baada ya hapo na makubaliano ni kuwa kilichoteremka baada ya muda wa Wahyi kukatika ni Suwrah hii (Al-Muddath-thir) kisha akatoa dalili ya hilo.

 

Na Haafidhw ametaja mfano wake katika Al-Fath (1/31)  na (10/304-305)

 

 

 Pia

 

وَحَدَّثَنَا زُهَيْرُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا الأَوْزَاعِيُّ، قَالَ سَمِعْتُ يَحْيَى، يَقُولُ سَأَلْتُ أَبَا سَلَمَةَ أَىُّ الْقُرْآنِ أُنْزِلَ قَبْلُ قَالَ: ((يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ)) ‏.‏ فَقُلْتُ أَوِ ((اقْرَأْ ))‏.‏ فَقَالَ سَأَلْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ أَىُّ الْقُرْآنِ أُنْزِلَ قَبْلُ قَالَ ((يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ)) ‏.‏ فَقُلْتُ أَوِ ((اقْرَأْ)) قَالَ جَابِرٌ أُحَدِّثُكُمْ مَا حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((جَاوَرْتُ بِحِرَاءٍ شَهْرًا فَلَمَّا قَضَيْتُ جِوَارِي نَزَلْتُ فَاسْتَبْطَنْتُ بَطْنَ الْوَادِي فَنُودِيتُ فَنَظَرْتُ أَمَامِي وَخَلْفِي وَعَنْ يَمِينِي وَعَنْ شِمَالِي فَلَمْ أَرَ أَحَدًا ثُمَّ نُودِيتُ فَنَظَرْتُ فَلَمْ أَرَ أَحَدًا ثُمَّ نُودِيتُ فَرَفَعْتُ رَأْسِي فَإِذَا هُوَ عَلَى الْعَرْشِ فِي الْهَوَاءِ )) يَعْنِي جِبْرِيلَ عَلَيْهِ السَّلاَمُ ((فَأَخَذَتْنِي رَجْفَةٌ شَدِيدَةٌ فَأَتَيْتُ خَدِيجَةَ فَقُلْتُ دَثِّرُونِي ‏.‏ فَدَثَّرُونِي فَصَبُّوا عَلَىَّ مَاءً فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ * قُمْ فَأَنْذِرْ * وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ * وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ)) ‏.‏

 

Zuhayr bin Harb ametuhadithia na Waliyd bin Muslim kadhalika na Al-Awzaa’iy amesema kuwa nimemsikia Yahyaa. Anasema nimemuuliza Abaa Salamah ni Qur-aan ipi iliyoteremka kabla akasema ni:

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika!

 

Nikasema au ni ((Iqraa?)). Akasema Nimemuuliza Jaabir bin Abdillaah ni Qur-aan ipi iliyoteremka kabla ya

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika!

 

Nikasema au ni ((Iqraa?))  Jaabir akasema: Niwahadithie alichohadithia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye amesema: “Nilikaa Hiraa muda wa mwezi mzima, nilipomaliza nikashuka Batwn Al-Waadiy nikawa ninaitwa nikaangalia upande wangu wa mbele kisha nyuma na kulia kisha kushoto sikuona chochote. Kisha nikaitwa tena nikaangalia sikuona yeyote kisha nikaitwa nikaangalia juu ya kichwa changu juu ya ‘Arsh hewani (yaaani Jibriyl عليه السلام) ikanipata mtetemeko mkubwa nikaenda kwa Khadiyjah nikamwambia: Dath-thiruwniy! (Yaani nigubikeni!). Hivyo wakanigubika na wakanimwagia maji. Baada ya hapo Allaah 'Azza wa Jalla Akateremsha:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika!

 

قُمْ فَأَنذِرْ﴿٢﴾

2. Simama na uonye 

 

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ﴿٣﴾

3. Na Rabb wako mtukuze. 

 

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ﴿٤﴾

4. Na nguo zako toharisha.

 

 

 

[Muslim Kitaab Al-Iymaan]

 

 

Aayah zinazoendelea:

 

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ﴿٥﴾

5. Na najisi (masanamu( epukana nayo.

 

 

وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ﴿٦﴾

6. Na wala usifanye fadhila kwa ajili ya kutaraji kukithirishiwa.

 

 

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ﴿٧﴾

7. Na kwa ajili ya Rabb wako subiri.

 

 

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ﴿٨﴾

8. Itakapopulizwa katika baragumu kwa sauti kali.

 

 

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ﴿٩﴾

9. Basi hiyo itakuwa ni Siku ngumu.

 

 

عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ﴿١٠﴾

10. Kwa makafiri si nyepesi.

 

 

 

 

Share