075 - Al-Qiyaamah

 

 

 

   الْقِيَامَة

Al-Qiyaamah: 075

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ﴿١﴾

1. Naapa kwa siku ya Qiyaamah.

 

 

وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa nafsi inayojilaumu sana.

 

 

أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ﴿٣﴾

3.  Je, anadhani binaadamu kwamba Hatutoikusanya mifupa yake?

 

 

بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ﴿٤﴾

4. Sivyo hivyo! Bali Tuna Uwezo wa kusawazisha sawasawa ncha za vidole vyake.

 

 

بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ﴿٥﴾

5. Bali anataka binaadamu aendelee kutenda dhambi na kukanusha umri wake ulobakia.

 

 

يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ﴿٦﴾

6. Anauliza ni lini hiyo siku ya Qiyaamah?

 

 

فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ﴿٧﴾

7. Basi jicho litakapoduwaa.

 

 

وَخَسَفَ الْقَمَرُ﴿٨﴾

8. Na mwezi utakapopatwa.

 

 

وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ﴿٩﴾

9. Na jua na mwezi vitakapojumuishwa.

 

 

يَقُولُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ﴿١٠﴾

10. Atasema binaadamu siku hiyo: Wapi pa kukimbilia?

 

 

كَلَّا لَا وَزَرَ﴿١١﴾

11. Laa hasha! Hapana mahali pa kimbilio.

 

 

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ﴿١٢﴾

12. Kwa Rabb wako siku hiyo ndio makazi ya kustakiri.

 

 

يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ﴿١٣﴾

13. Siku hiyo binaadamu atajulishwa yale aliyoyakadimisha na aliyoyaakhirisha.

 

 

بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ﴿١٤﴾

14. Bali binaadamu ni shahidi dhidi ya nafsi yake.

 

 

وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ﴿١٥﴾

15. Japo akitoa nyudhuru zake zote.

 

 

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾

16. Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

 

 

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ﴿١٧﴾

17. Hakika ni juu Yetu Kuikusanya na Kukuwezesha kuisoma kwake.

 

 

فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ﴿١٨﴾

18. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake.

 

 

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ﴿١٩﴾

19. Kisha ni juu Yetu Kuibainisha (kwako).

 

 

كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ﴿٢٠﴾

20. Laa hasha! Bali mnapenda uhai wa dunia.

 

 

وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ﴿٢١﴾

21. Na mnaiacha Aakhirah.

 

 

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ﴿٢٢﴾

22.  Nyuso siku hiyo zitanawiri.

 

 

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ﴿٢٣﴾

23. Zikimtazama Rabb wake.

                                                                            

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ﴿٢٤﴾

24. Na nyuso (nyenginezo) siku hiyo zitakunjana.

 

 

تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ﴿٢٥﴾

25. Zikiwa na yakini kuwa zitafikiwa na msiba unaovunja uti wa mgongo.

 

 

كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ﴿٢٦﴾

26. Laa hasha! Itakapofika (roho) mafupa ya koo.

 

 

وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ﴿٢٧﴾

27. Na itasemwa:  Ni nani tabibu wa kumponya?

 

 

وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ﴿٢٨﴾

28. Na atakuwa na yakini kwamba hakika hivyo ni kufariki.

 

 

وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ﴿٢٩﴾

29. Na muundi utakapoambatana na muundi.

 

 

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ﴿٣٠﴾

30. Siku hiyo ni kuendeshwa na kupelekwa kwa Rabb wako tu.

 

 

 

فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ﴿٣١﴾

31. Kwani hakusadiki (Qur-aan na Rasuli) na wala hakuswali.

 

 

وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ﴿٣٢﴾

32. Lakini alikadhibisha na akakengeuka.

 

 

ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰ أَهْلِهِ يَتَمَطَّىٰ﴿٣٣﴾

33. Kisha akaenda kwa watu wake akijigamba.

 

 

أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٤﴾

34. Ole kwako! Tena ole kwako (ewe kafiri)!

 

 

ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٥﴾

35. Kisha ole kwako! Tena ole kwako!

 

 

 

أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى﴿٣٦﴾

36. Je, anadhani binaadamu ataachwa huru bila jukumu?

 

 

أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ﴿٣٧﴾

37. Kwani hakuwa tone kutokana na manii yanayomwagwa kwa nguvu?

 

 

ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ﴿٣٨﴾

38. Kisha akawa pande la damu, (Allaah) Akamuumba na Akamsawazisha?

 

 

فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ﴿٣٩﴾

39. Akamfanya namna mbili; mwanamume na mwanamke?

 

 

 

أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ﴿٤٠﴾

40. Je Huyo (Allaah Anayeumba) Si Muweza wa Kuhuisha wafu?!  

 

 

 

 

Share