Mikate Ya Naan Ya Mtindi Katika Mkaa

 

Mikate Ya Naan Ya Mtindi Katika Mkaa  

 

Kupata Kiasi Mikate 12

Vipimo

Unga - Magi 4 (mug)

Mtindi (Yoghurt) - 1 magi

Hamira ya chenga ya tayari (instant) - 1 kijiko cha supu

Mafuta - 1 kijiko cha supu

Maji - 1 magi

Chumvi - 1 kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya unga, hamira na chumvi katika sinia.


  2. Tia mafuta na mtindi uchanganye vizuri.


  3. Tia maji uchanganye na kukanda uwe kama unga wa chapati/mkate wa kusukuma.


  4. Fanya madonge kisha sukuma, kisha weka mkate baina ya wavu mbili na choma katika mkaa


  5. Ukiiva pande zote mbili, weka katika sahani ya kupakulia upake siagi.

 Wavu mbili wa kuchomea vyakula juu ya makaa

 

 

 

 

 

Share