Amiyr Wa Waumini 'Umar Bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'Anhu) - Fadhila Za Kusema 'Jazaaka Allaahu khayraa' (Allaah Akulipe khayr)

Fadhila Za Kusema 'Jazaaka Allaahu khayra' (Allaah Akulipe khayr)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Amiyr wa Waumini, 'Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema:

 

"Angalikuwa mmoja wenu anaelewa malipo ya kumwambia ndugu yake 'Jazaaka Allaahu khayra' (Allaah Akulipe khayr), basi kwa hakika mngeliambiana kila wakati."

[Al-Muswanaf, Ibn Abiy Shaybah 26519]

 

Shaykh 'Abdur-Razaaq Al-Badr, anasema (kufafanua athar hiyo ya Amiyr wa Waumini):

 

"Ni makubwa kiasi gani kwa uzito maneno haya, na yenye nguvu na kumshajiiisha yule mwenye kufanya wema; kwa sababu neno hili linadhihirisha mipaka na kutoweza kumlipa yule mtu (aliyekufanyia wema) na hivyo kuelekeza malipo kwa Allaah ili Yeye Amlipe huyo mtu badala yako wewe, kwa ujira uliokamilika kabisa.

 

Kama wanavyosema baadhi ya watu: Ikiwa mkono wako ni 'mfupi' sana katika kulipa fadhila, basi uache ulimi wako uwe 'mrefu' kwa kutoa shukurani na kwa du'aa  kumuombea (mwenzako aliyekufanyia wema) ujira na malipo."

[Athar wa Ta'liyq]

 

 

Share