Pai Za Kuku Na Kabichi

Pai Za Kuku Na Kabeji

 

Vipimo

Unga wa kitobosha (puff pastry) - 12 – 15 vipande

Kidari cha kuku - ½ kilo

Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya kulia

Thomu (saumu, garlic) - 1 kijiko cha kulia

Pilipili manga - 2 vijiko vya chai

Ndimu - 3 kiasi kamua

Mdalasini - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Kabichi (cabbage) - ½ Nusu

Yai - 1

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Unga wa vitobosho (Puff pastry) utoe mapema katika freezer.
  2. Washa oveni mapema moto wa kiasi 200 Degrees (inategemea na aina ya oveni)
  3. Katakata kuku vipande kiasi weka katika sufuria.
  4. Tia viungo vyote kisha funika apikike kuku kwa viungo. Ikibid kuongeza maji kidogo ongeza awive kuku.
  5. Epua, kisha chambua chambua kuku.
  6. Katakataka kabichi nyembamba utie uchanganye vizuri. Kolezea ndimu, pilipili manga na chumvi na bizari ukipenda.
  7. Fungua puff pastry moja weka mchanganyiko kiasi katikati.

      8. Kunja pembeni kisha bania kwa uma ufanye design.

      9. Panga katika treya uliyopaka siagi ili visigande.

    10. Pakaza yai

    11. Weka katika oveni uoke (Bake) kwa muda wa dakika 10 – 15 mpaka vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)

    12. Epua vikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

Share