Vitobosha (Croissant ) Vya Nyama

Vitobosha (Croissant ) Vya Nyama

Vipimo

Siagi  - 1Kg

unga wa ngano - 2 ½ Kg

Cheez wheez - 3 Vijiko vikubwa vya chai

Hamira   - 1 kijiko cha chai

Nyama  - 1 Kg

Vitunguu saumu(thomu) - 1 kijiko cha chai

Tangawizi - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Uzile(cumin powder)  - 1 kijiko cha chai

Chumvi   - kiasi

Mayai  - 2

Maziwa - 1 kikombe

Namna ya Kutayarisha

  1. Changanya nyama, tangawizi, thomu, pilipili manga,   uzile na chumvi.Iweke jikoni na kukoroga bila ya kutia maji mpaka ikauke. ( hakikisha imekuwa kavu)
  2. Roweka hamira kwenye maji ya robo kikombe.
  3. Changanya vizuri siagi na cheese.
  4. Mimina unga kwenye mchanganyiko wa siagi na uchanganye vizuri.
  5. Mimina hamira kwenye unga pamoja na maziwa
  6. Uchanganye vizuri bila ya kuukanda, unaweza kuongeza maji kama hayakutosha (usiwe umaji kama unga wa chapati)
  7. Kata madonge na usukume kama chapati, kata sehemu nne, chukua kipande kimoja ukifanye umbo la sambusa, lakini pembe moja ifanye ndefu, chukua nyama kijiko 1 uweke juu yake na ikunjie kuanzia upande ulioweka nyama, yaani kamata ncha moja kulia na moja kushoto ikunjie nyama kwa kuelekea kwenye ile ncha ndefu, halafu ipinde ili upate umbo kama kwenye picha. Endelea kufanya hivyo mpaka umalize zote.
  8. Piga mayai kwenye kibakuli, chukua brushi ya kupakia na uzipake mayai juu yake.
  9. Zichome kwenye oven na moto wa 350’F, mpaka zibadilike rangi.
  10. Zitoe weka kwenye sahani tayari kwa kula.

 

 

 

 

 

Share