Pai Za Nyama Na Mboga Ya Karoti

Pai Za Nyama Na Mboga Ya Karoti   

Vipimo

Unga Wa Kitobosha (puff pastry) - 30 kiasi vipande

Nyama ya kusaga - 1 Lb (ratili)

Kitunguu saumu(thomu) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipilimanga - 1 kijiko cha chai

Pilipili mbichi iliyosagwa -  1 kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha cha

Ndimu - 2 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Jiyra (cumin powder) -  ½ kijiko cha chai

Kitunguu - 1 kimoja

Karoti - 1

Kotmiri -  ½ kikombe cha chai

Kiazi   kilochemshwa - 1

Mayai 2  au maziwa ya chai mazito kwa ajili ya kupakaza juu ya pai.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika sufuria weka nyama ya kusaga, tia thomu na tangawizi iliyosagwa, bizari zote, pilipili zote, ndimu, chumvi kisha iache ipikike kama nyama ya sambusa. Zima moto weka kando.
  2. Katakata kitunguu, chuna karoti, katakata kotmiri, kisha changanya pamoja na nyama.
  3. Ponda kiazi kilochemshwa uchanganye na mchanganyiko ukiwa tayari kujazwa katika unga wa kitobosha.

  

    

     4. Jaza kama katika picha, kisha kunja upendavyo, ikiwa ni pembe tatu kama sambusa au kunja mstatili (rectangle)

     5. Bana pembe zote kwa umma .

 

     

     6. Paka sigai treya ya kupikia katika oveni, zipange pai.

     7. Piga mayai katika kibakuli au tumia maziwa, kisha pakaza juu ya  pai kwa kutumia brashi (brush) ndogo,na uzichome (Bake) katika oveni kwa moto wa takriban 350°C kwa muda wa ½ saa au hadi zibakilike rangi na kuiva.

     8. Epua zipange katika sahani zikiwa tayari.

Kidokezo:

Unga wa vitobosho unaweza kununua wa tayari wa kiasi cha gram 400 kisha ukate vipande vipande.

 

 

 

Share