Kulfi

Kulfi

Vipimo:

Maziwa ya mvuke (evaporated milk) -  3 kopo

Maziwa ya mazito (condensed milk) - 1 kopo

Malai ya Maziwa (cream milk/Qishtwah) -  1 kopo

Malai yenye siagi yaliyopigwapigwa

yakawa mazito (cool whip) - 1 kopo

Zafaraani -  1/2 kijiko cha chai

Hiliki -   1/4 kijiko cha chai

Lozi za vipande -   1/2  kikombe

Lozi ya unga -   1/4 kikombe 

Njugu (Pistachio) zilizokatwa katwa -  1/2 kikombe         

Namna ya Kutayarisha:

  1. Katika bakuli, changanya evaporated milk, condensed milk na cream milk.
  2. Koroga taratibu mpaka ichanganyike.
  3. Tia hiliki na zafarani changanya tena vizuri.
  4. Mwisho mimina cool whip koroga ikisha kuwa nzito imimine kwenye bakuli na nyunyizia lozi ya vipande, ya unga na pistachio.
  5. Tia kwenye freezer iache igande kwa muda wa siku nzima au zaidi. 
  6. Itoe na itakuwa tayari kuliwa. Kata kata vipande tia kwenye vibakuli au visahani. Iliyobakia ihifadhi katika friji hadi utakapoihitaji kuila tena. 
Share