Pakoras (Bajia) Za Bilingani Na Viazi Kwa Salsa Ya Uwatu

Pakoras Bajia Za Bilingani, Viazi Kwa Salsa Ya Uwatu

 

Vipimo 

Bilingani 1 katakata vipande vidogodogo

Viazi 2 katakata vipande vidodogo vyembamba

Kitunguu 1 katakata slice za kiasi

Kotmiri msongo (bunch) moja ndogo katakata

Pilipili mbichi 1 katakata ndogo ndogo

Jira/bizari nzima/cumin 1 kijiko cha chai

Chumvi kijiko 1 cha chai

Haldi/bizari ya manjano (turmeric) ½ kijiko cha chai

Uwatu wa unga (methi/fenugreek) ½ kijiko cha chai

Unga wa dengu kikombe 1

Maji ½ kikombe

Mafuta ya kukaangia

 

 

Vipimo Vya Salsa

 

Pilipili kubwa tamu (capsicum)

Nyanya 2

Thomu (saumu/garlic) chembe 3

Pilipili mbichi 2

Uwatu (methi/fenugreek) 1 kijiko cha chai

Siki au ndimu vijiko vya kulia

Chumvi kiasi

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Changanya vizuri vitu vyote vya bajia katika bakuli.
  2. Weka mafuta katika karai yaache yashike moto. Chota kwa kijiko cha kulia au kwa mkono mchanganyiko wa bajia ukaange katika mafuta.
  3. Kaanga mpaka zigeuke rangi.
  4. Epua uchuje mafuta kwenye chujio kisha weka katika kitchen tissues zizidi kuchuja mafuta.
  5. Panga katika sahani zikiwa tayari.

 

Salsa Ya Nyanya Pilipili Tamu Na Uwatu

 

 

  1. Katakata vitu katika mashine ya kusagia (blender) usage vizuri.
  2. Mimina katika bakuli utolee la pakoras (bajia)

 

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share