Kabaab Za Nyama Za Kukaanga Za Slaisi Ya Mkate

Kabaab Za Nyama Za Kukaanga Za Slaisi Ya Mkate

Vipimo

Nyama ya kusaga - 1 kilo moja

Slaisi za mkate - 5

Mayai - 2

Unga wa dengu - 1 kijiko cha supu

Kitunguu katakata (chopped) - 1 kikubwa

Tangawizi ya kusagwa - 2 vijiko vya supu

Thomu (garlic/saumu) ilosagwa - 1 kijiko

Pilipili mbichi katakata (chopped) - 2 chembe

Bizari mchanganyiko - 2 vijiko vya chai

Kotmiri freshi ilokatwakatwa - kikombe kimoja

Chumvi - kiasi

Mafuta ya kukaangia.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka slaisi za mkate katika bakuli lenye maji, roweka kisha kamua vizuri mkate.
  2. Piga mayai katika kibakuli.
  3. Changanya nyama na vitu vyote.
  4. Chota kidonge kiasi uchome katika mafuta makali, zikitokea kuwa ni ngumu basi ongeza yai au zikiwa ni laini mno, basi ongezea unga wa dengu zishikamane.
  5. Kisha fanya madonge nyama yote.
  6. Choma katika mafuta uepuea kuchuja mafuta zikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share