Crapes Kwa Asali

Crapes Kwa Asali

 

Vipimo   

 

Unga kikombe 1 ½

Baking powder 2 vijiko vya chai

Yai 1

Sukari vijiko 2 vya kulia

Maziwa kikombe 1

Siagi isiyo ya chumvi (butter) vijiko 2 vya kulia

Mafuta 1 kijiko cha kulia

Chumvi ¼ kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya katika bakuli, unga, sukari, baking powder na chumvi  
  2. Changanya yai na maziwa kisha mimina katika bakuli uchanganye vyote pamoja upige vizuri kwa mchapo (Whisk).
  3. Weka chuma kisichoganda (non-stick pan) katika moto, Paka samli kidogo kisha teka mteko kwa upawa umimine ufanye kiduara.
  4. Itakapoanza kufanya vibofu (bubbles) geuza upande wa pili .
  5. Tia samli kidogo, upike hadi igeuke rangi ya hudhurungi.
  6. Epua weka katika sahani, endelea kumalilzia kupika crapes zote.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

Kidokezo : Nzuri kula asubuhi (Breakfast) pamoja na yai kando yake.

 

 

Share