Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Waarabu Hawatofanikiwa Kuirejesha Ardhi Ya Palestina Kwa Uarabu Bali Kwa Uislamu

Waarabu Hawatofanikiwa Kuirejesha Ardhi Ya Palestina Kwa Uarabu Bali Kwa Uislamu

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Hawatofanikiwa abadan Waarabu kwa ninavyoitakidi -Na elimu iko kwa Allaah- kuirejesha ardhi ya Palestina kwa kutumia jina la Uarabu. Na haiwezekani kuirejesha isipokuwa kwa jina la Uislamu kwa (Manhaj) aliyokuwa nayo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake.

 

Kama Alivyosema Ta’aalaa:

“…Hakika ardhi ni ya Allaah; Humrithisha Amtakaye katika wa waja Wake. Na mwisho (mzuri) ni kwa wenye taqwa.” [Al-A’raaf: 128]

 

 

[Tafsiyr Suwrat Al-Baqarah Libn ‘Uthaymiyn, mj. 1, uk. 169-170]

 

Alhidaaya.com   

 

 

Share