Kauli Za Salaf: Taqwa-Ikhlaasw
Kinofu Cha Mwili Akipendacho Mno Allaah Na Akichukiacho Ni Ulimi…
Imaam Fudhwayl Bin ‘Iyaadhw (Rahimahu Allaah)
Imaam Fudhwayl Bin ‘Iyaadhw (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakuna kinofu cha mwili Akipendacho Allaah kama ulimi usemao kweli, na hakuna kinofu cha mwili Akichukiacho Allaah kama ulimi usemao uongo.”
[Rawdhwah Al-‘Uqalaa li-Abiy Haatim Al-Bustiy (Uk. 52)]