Viazi Vya Jibini Na Maziwa

Vipimo
Viazi 7-9
Maziwa ya kopo(evaporated milk) 1 mkebe
Unga wa ngano ½ kikombe cha chai
Siagi 4 vijiko vya chakula
Chumvi kiasi
Namna Yakutayarisha
1. Anza kuwasha oveni moto wa 350°F.
2. vioshe viazi vizuri na maganda yake kisha kata slesi za duara.
3. halafu pakaza siagi kwenye treya ya kuchomea na panga slesi za viazi zikiwa zinakaliana juu ya slesi nyingine.
4. kisha mimina maziwa ya kopo kiasi kuziba ziba kila kiazi.
5. Kisha nyunyizia chumvi na nyunyizia na unga kijiko kimoja halafu dondoshea siagi au butter matone matone kwenye treya yote juu ya viazi.
6. kisha panga tena viazi juu yake
7. Halafu malizia juu kumimina maziwa yote yaliyobaki.
8. kwa ladha nzuri badala ya maziwa ya kopo ni bora kunyunyizia urojo wa bashameli.(tazama kwenye macaroni ya bashameli kupata vipimo na kutayarisha bashameli)
9. mwisho tia kwenye oven kwa muda wa dakika 30-45 au mpaka viazi viwive vizuri. Epua na tayari kwa kuliwa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
