Mboga Mchanganyiko

VIPIMO:
Brokoli (Brocoli) 1 mche
Karoti 3
Viazi 2
Njegere (snow-peas) au zozote 1 kikombe
Zuchini (
Pililipili mboga za rangi mbali mbali 1 kila rangi
Kidonge cha supu (Maggi cube) 1
Pilipili manga 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Sosi ya soy 1 kijiko cha supu
Mafuta ya kukaangia 1/4 kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Kata kwanza viazi, zuchini na karoti vipande virefu verefu kisha chemsha kidogo tu. Tia chumvi na pilipili manga.
2. Tia mafuta katika karai, kaanga vitu vyote isipokuwa brokoli na mapilipili makubwa.
3. Karibu na kuwiva tia sosi ya soy na kidonge cha supu.
4. Kata au chambua brokoli, kata kata mapilipili na tia katika mchangayiko, ipikike muda wa dakika tano tu. Changanya vizuri, tayari kuliwa na mkate au wali mweupe.
Kidokezo:
Usikaange au kuchemsha
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


