Fasulia (Maharage) Za Kukaanga

Vipimo
Maharage 1 Kopo
Kitunguu 1
Nyanya 1 Kubwa
Pilipili mbichi 1- 2
Nyanya ya kopo ½ Kijiko cha chai
Pilipili ya unga ¼ Kijiko
Chumvi Kiasi
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Kidonge cha supu ½ Kidonge
Mafuta ya zaituni 4 Vijiko vya supu
Maji Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka maharage, kisha chemsha hadi yawive na kulainika; ikiwa unatumia maharage ya mkebe hakikisha unayaosha kwanza.
- Katika sufuria, tia mafuta na kaanga kitunguu na thomu mpaka ibadilike rangi na sio kuungua.
- Kisha tia nyanya (tungule) aina zote mbili, pilipili ya unga na pilipili mbichi, kidonge cha supu na maharage na ufunike na iache katika moto wa kiasi na usikoroge.
- Yakisha kaangika, utayaponda ponda, kisha tia maji ya kiasi na iache itokote kidogo.
- Halafu epua motoni na itakuwa tayari kwa kuliwa na mkate au chapati.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
